Luke 24
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 On the first day of the week, very early in the morning, the women came to the tomb, bringing the spices they had prepared. | SWKCV 1 Mnamo siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa, wakaenda kaburini. |
| BSB 2 They found the stone rolled away from the tomb, | SWKCV 2 Wakakuta lile jiwe limevingirishwa kutoka kwenye kaburi, |
| BSB 3 but when they entered, they did not find the body of the Lord Jesus. | SWKCV 3 lakini walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Yesu. |
| BSB 4 While they were puzzling over this, suddenly two men in radiant apparel stood beside them. | SWKCV 4 Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayongʼaa kama umeme wakasimama karibu nao. |
| BSB 5 As the women bowed their faces to the ground in terror, the two men asked them, “Why do you look for the living among the dead? | SWKCV 5 Wale wanawake, wakiwa na hofu, wakainamisha nyuso zao mpaka chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? |
| BSB 6 He is not here; He has risen! Remember how He told you while He was still in Galilee: | SWKCV 6 Hayuko hapa; amefufuka! Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa bado yuko pamoja nanyi huko Galilaya kwamba: |
| BSB 7 ‘The Son of Man must be delivered into the hands of sinful men, and be crucified, and on the third day rise again.’” | SWKCV 7 ‘Ilikuwa lazima Mwana wa Adamu atiwe mikononi mwa watu wenye dhambi na waovu ili asulubiwe, na siku ya tatu afufuke.’” |
| BSB 8 Then they remembered His words. | SWKCV 8 Ndipo wakayakumbuka maneno ya Yesu. |
| BSB 9 And when they returned from the tomb, they reported all these things to the Eleven and to all the others. | SWKCV 9 Waliporudi kutoka huko kaburini, wakawaeleza wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na wengine wote mambo haya yote. |
| BSB 10 It was Mary Magdalene, Joanna, Mary the mother of James, and the other women with them who told this to the apostles. | SWKCV 10 Basi Maria Magdalene, Yoana, na Maria mama yake Yakobo, pamoja na wanawake wengine waliofuatana nao ndio waliwaelezea mitume habari hizi. |
| BSB 11 But their words seemed like nonsense to them, and they did not believe the women. | SWKCV 11 Lakini hawakuwasadiki hao wanawake, kwa sababu maneno yao yalionekana kama upuzi. |
| BSB 12 Peter, however, got up and ran to the tomb. And after bending down and seeing only the linen cloths, he went away, wondering to himself what had happened. | SWKCV 12 Hata hivyo, Petro akainuka na kukimbia kwenda kule kaburini. Alipoinama kuchungulia, akaona vile vitambaa vya kitani, ila hakuona kitu kingine. Naye akaenda zake akijiuliza nini kilichotokea. |
| BSB 13 That same day two of them were going to a village called Emmaus, about seven miles from Jerusalem. | SWKCV 13 Ikawa siku iyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa njiani wakienda kijiji kilichoitwa Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu. |
| BSB 14 They were talking with each other about everything that had happened. | SWKCV 14 Walikuwa wakizungumza wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotukia. |
| BSB 15 And as they talked and deliberated, Jesus Himself came up and walked along with them. | SWKCV 15 Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Yesu mwenyewe akaja akatembea pamoja nao, |
| BSB 16 But their eyes were kept from recognizing Him. | SWKCV 16 lakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue. |
| BSB 17 He asked them, “What are you discussing so intently as you walk along?” They stood still, with sadness on their faces. | SWKCV 17 Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumza wakati mnatembea?” Wakasimama, nyuso zao zikionyesha huzuni. |
| BSB 18 One of them, named Cleopas, asked Him, “Are You the only visitor to Jerusalem who does not know the things that have happened there in recent days?” | SWKCV 18 Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamuuliza, “Je, wewe ndiye peke yako mgeni huku Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotukia humo siku hizi?” |
| BSB 19 “What things?” He asked. “The events involving Jesus of Nazareth,” they answered. “This man was a prophet, powerful in speech and action before God and all the people. | SWKCV 19 Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu, “Mambo ya Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii, mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele ya wanadamu wote. |
| BSB 20 Our chief priests and rulers delivered Him up to the sentence of death, and they crucified Him. | SWKCV 20 Viongozi wa makuhani na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa, nao wakamsulubisha. |
| BSB 21 But we were hoping He was the One who would redeem Israel. And besides all this, it is the third day since these things took place. | SWKCV 21 Lakini tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angelikomboa Israeli. Zaidi ya hayo, leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee. |
| BSB 22 Furthermore, some of our women astounded us. They were at the tomb early this morning, | SWKCV 22 Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtusha. Walikwenda kaburini leo alfajiri, |
| BSB 23 but they did not find His body. They came and told us they had seen a vision of angels, who said that Jesus was alive. | SWKCV 23 lakini hawakuukuta mwili wake. Walirudi wakasema wameona maono ya malaika ambao waliwaambia kwamba Yesu yu hai. |
| BSB 24 Then some of our companions went to the tomb and found it just as the women had described. But Him they did not see.” | SWKCV 24 Kisha baadhi ya wenzetu walikwenda kaburini wakalikuta kama vile wale wanawake walivyokuwa wamesema, lakini yeye hawakumwona.” |
| BSB 25 Then Jesus said to them, “O foolish ones, and slow of heart to believe all that the prophets have spoken! | SWKCV 25 Yesu akawaambia, “Ninyi ni wajinga kiasi gani, nanyi ni wazito mioyoni mwenu kuamini mambo yote yaliyonenwa na manabii! |
| BSB 26 Was it not necessary for the Christ to suffer these things and then to enter His glory?” | SWKCV 26 Je, haikumpasa Kristo kuteswa kwa njia hiyo na kisha aingie katika utukufu wake?” |
| BSB 27 And beginning with Moses and all the Prophets, He explained to them what was written in all the Scriptures about Himself. | SWKCV 27 Naye akianzia na Sheria ya Mose na Manabii wote, akawafafanulia jinsi Maandiko yalivyosema kumhusu yeye. |
| BSB 28 As they approached the village where they were headed, He seemed to be going farther. | SWKCV 28 Nao walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea mbele. |
| BSB 29 But they pleaded with Him, “Stay with us, for it is nearly evening and the day is almost over.” So He went in to stay with them. | SWKCV 29 Lakini wao wakamsihi sana akae nao, wakisema, “Kaa hapa nasi, kwa maana sasa ni jioni na usiku unaingia.” Basi akaingia ndani kukaa nao. |
| BSB 30 While He was reclining at the table with them, He took bread, spoke a blessing and broke it, and gave it to them. | SWKCV 30 Alipokuwa mezani pamoja nao, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. |
| BSB 31 Then their eyes were opened and they recognized Jesus—and He disappeared from their sight. | SWKCV 31 Ndipo macho yao yakafumbuliwa, nao wakamtambua, naye akatoweka machoni pao. Hawakumwona tena. |
| BSB 32 They asked each other, “Were not our hearts burning within us as He spoke with us on the road and opened the Scriptures to us?” | SWKCV 32 Wakaulizana wao kwa wao, “Je, mioyo yetu haikuwakawaka kwa furaha ndani yetu alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?” |
| BSB 33 And they got up that very hour and returned to Jerusalem. There they found the Eleven and those with them, gathered together | SWKCV 33 Wakaondoka mara, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusanyika |
| BSB 34 and saying, “The Lord has indeed risen and has appeared to Simon!” | SWKCV 34 wakisema, “Ni kweli! Bwana amefufuka, naye amemtokea Simoni.” |
| BSB 35 Then the two told what had happened on the road, and how they had recognized Jesus in the breaking of the bread. | SWKCV 35 Kisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotukia njiani na jinsi walivyomtambua Yesu alipoumega mkate. |
| BSB 36 While they were describing these events, Jesus Himself stood among them and said, “Peace be with you.” | SWKCV 36 Walipokuwa bado wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasimama katikati yao, akasema, “Amani iwe nanyi!” |
| BSB 37 But they were startled and frightened, thinking they had seen a spirit. | SWKCV 37 Wakashtuka na kuogopa wakidhani kwamba wameona mzuka. |
| BSB 38 “Why are you troubled,” Jesus asked, “and why do doubts arise in your hearts? | SWKCV 38 Lakini Yesu akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna shaka mioyoni mwenu? |
| BSB 39 Look at My hands and My feet. It is I Myself. Touch Me and see—for a spirit does not have flesh and bones, as you see I have.” | SWKCV 39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, mwone kuwa ni mimi hasa. Niguseni mwone; kwa maana mzuka hauna nyama na mifupa, kama mnionavyo kuwa navyo.” |
| BSB 40 And when He had said this, He showed them His hands and feet. | SWKCV 40 Aliposema haya, akawaonyesha mikono na miguu yake. |
| BSB 41 While they were still in disbelief because of their joy and amazement, He asked them, “Do you have anything here to eat?” | SWKCV 41 Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula chochote hapa?” |
| BSB 42 So they gave Him a piece of broiled fish, | SWKCV 42 Wakampa kipande cha samaki aliyeokwa, |
| BSB 43 and He took it and ate it in front of them. | SWKCV 43 naye akakichukua na kukila mbele yao. |
| BSB 44 Jesus said to them, “These are the words I spoke to you while I was still with you: Everything must be fulfilled that is written about Me in the Law of Moses, the Prophets, and the Psalms.” | SWKCV 44 Akawaambia, “Haya ndiyo yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Sheria ya Mose, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.” |
| BSB 45 Then He opened their minds to understand the Scriptures. | SWKCV 45 Ndipo akafungua fahamu zao ili waweze kuyaelewa Maandiko. |
| BSB 46 And He told them, “This is what is written: The Christ will suffer and rise from the dead on the third day, | SWKCV 46 Akawaambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. |
| BSB 47 and in His name repentance and forgiveness of sins will be proclaimed to all nations, beginning in Jerusalem. | SWKCV 47 Toba na msamaha wa dhambi zitatangaziwa mataifa yote kupitia jina lake kuanzia Yerusalemu. |
| BSB 48 You are witnesses of these things. | SWKCV 48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya. |
| BSB 49 And behold, I am sending the promise of My Father upon you. But remain in the city until you have been clothed with power from on high.” | SWKCV 49 “Tazama nitawatumia ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini hadi mtakapovikwa uwezo utokao juu.” |
| BSB 50 When Jesus had led them out as far as Bethany, He lifted up His hands and blessed them. | SWKCV 50 Akiisha kuwaongoza mpaka kwenye viunga vya Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki. |
| BSB 51 While He was blessing them, He left them and was carried up into heaven. | SWKCV 51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni. |
| BSB 52 And they worshiped Him and returned to Jerusalem with great joy, | SWKCV 52 Kisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu. |
| BSB 53 praising God continually in the temple. | SWKCV 53 Nao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu. Amen. |
Questions about Luke 24? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.