Mark 4
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Once again Jesus began to teach beside the sea, and such a large crowd gathered around Him that He got into a boat and sat in it, while all the people crowded along the shore. | SWKCV 1 Yesu akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Umati wa watu uliokuwa umekusanyika kumzunguka ulikuwa mkubwa, kiasi kwamba ilimbidi Yesu aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo, nao watu wote walikuwa ufuoni mwa bahari. |
| BSB 2 And He taught them many things in parables, and in His teaching He said, | SWKCV 2 Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema: |
| BSB 3 “Listen! A farmer went out to sow his seed. | SWKCV 3 “Sikilizeni! Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. |
| BSB 4 And as he was sowing, some seed fell along the path, and the birds came and devoured it. | SWKCV 4 Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. |
| BSB 5 Some fell on rocky ground, where it did not have much soil. It sprang up quickly because the soil was shallow. | SWKCV 5 Nyingine zilianguka kwenye ardhi yenye mwamba isiyo na udongo wa kutosha. Zikaota haraka, kwa kuwa udongo ulikuwa haba. |
| BSB 6 But when the sun rose, the seedlings were scorched, and they withered because they had no root. | SWKCV 6 Lakini jua lilipozidi, mimea ikanyauka na kukauka kwa kuwa mizizi yake haikuwa na kina. |
| BSB 7 Other seed fell among thorns, which grew up and choked the seedlings, and they yielded no crop. | SWKCV 7 Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo miiba hiyo ikakua, ikaisonga hiyo mimea, hivyo haikutoa mazao. |
| BSB 8 Still other seed fell on good soil, where it sprouted, grew up, and produced a crop—one bearing thirtyfold, another sixtyfold, and another a hundredfold.” | SWKCV 8 Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri, zikaota vizuri na kukua, zikatoa mazao, moja mara thelathini, nyingine mara sitini, na nyingine mara mia moja.” |
| BSB 9 Then Jesus said, “He who has ears to hear, let him hear.” | SWKCV 9 Kisha Yesu akasema, “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” |
| BSB 10 As soon as Jesus was alone with the Twelve and those around Him, they asked Him about the parable. | SWKCV 10 Alipokuwa peke yake, watu waliokuwepo naye pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili wakamuuliza kuhusu mifano yake. |
| BSB 11 He replied, “The mystery of the kingdom of God has been given to you, but to those on the outside everything is expressed in parables, | SWKCV 11 Naye akawaambia, “Ninyi mmepewa kujua siri ya Ufalme wa Mungu. Lakini kwa wale walioko nje, kila kitu husemwa kwao kwa mifano, |
| BSB 12 so that, ‘they may be ever seeing but never perceiving, and ever hearing but never understanding; otherwise they might turn and be forgiven.’” | SWKCV 12 ili, “ ‘daima waone lakini wasitambue, daima wasikie lakini wasielewe; wasije wakageuka, wakatubu na kusamehewa!’” |
| BSB 13 Then Jesus said to them, “Do you not understand this parable? Then how will you understand any of the parables? | SWKCV 13 Kisha Yesu akawauliza, “Hamwelewi maana ya mfano huu? Basi mtaelewaje mifano mingine? |
| BSB 14 The farmer sows the word. | SWKCV 14 Yule mpanzi hupanda neno. |
| BSB 15 Some are like the seeds along the path, where the word is sown. As soon as they hear it, Satan comes and takes away the word that was sown in them. | SWKCV 15 Hawa ndio wale walio kando ya njia ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, Shetani huja mara na kulinyakua lile neno lililopandwa ndani yao. |
| BSB 16 Some are like the seeds sown on rocky ground. They hear the word and at once receive it with joy. | SWKCV 16 Nazo zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, ni wale wanaolisikia neno, na mara hulipokea kwa furaha. |
| BSB 17 But they themselves have no root, and they remain for only a season. When trouble or persecution comes because of the word, they quickly fall away. | SWKCV 17 Lakini kwa kuwa hawana mizizi, wao hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, mara wao huiacha imani. |
| BSB 18 Others are like the seeds sown among the thorns. They hear the word, | SWKCV 18 Lakini wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba, hulisikia lile neno; |
| BSB 19 but the worries of this life, the deceitfulness of wealth, and the desire for other things come in and choke the word, and it becomes unfruitful. | SWKCV 19 lakini masumbufu ya maisha haya, na udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae. |
| BSB 20 Still others are like the seeds sown on good soil. They hear the word, receive it, and produce a crop—thirtyfold, sixtyfold, or a hundredfold.” | SWKCV 20 Wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri, hulisikia lile neno, wakalipokea na kuzaa mazao. Wao huzaa mara thelathini, au mara sitini, au mara mia ya mbegu iliyopandwa.” |
| BSB 21 Jesus also said to them, “Does anyone bring in a lamp to put it under a basket or under a bed? Doesn’t he set it on a stand? | SWKCV 21 Akawaambia, “Je, taa huwashwa na kufunikwa chini ya kikapu au mvunguni mwa kitanda? Je, haiwashwi na kuwekwa juu ya kinara chake? |
| BSB 22 For there is nothing hidden that will not be disclosed, and nothing concealed that will not be brought to light. | SWKCV 22 Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni. |
| BSB 23 If anyone has ears to hear, let him hear.” | SWKCV 23 Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” |
| BSB 24 He went on to say, “Pay attention to what you hear. With the measure you use, it will be measured to you, and even more will be added to you. | SWKCV 24 Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi. |
| BSB 25 For whoever has will be given more. But whoever does not have, even what he has will be taken away from him.” | SWKCV 25 Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa.” |
| BSB 26 Jesus also said, “The kingdom of God is like a man who scatters seed on the ground. | SWKCV 26 Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. |
| BSB 27 Night and day he sleeps and wakes, and the seed sprouts and grows, though he knows not how. | SWKCV 27 Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo. |
| BSB 28 All by itself the earth produces a crop—first the stalk, then the head, then grain that ripens within. | SWKCV 28 Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke. |
| BSB 29 And as soon as the grain is ripe, he swings the sickle, because the harvest has come.” | SWKCV 29 Lakini nafaka inapokuwa imekomaa, mara mkulima huingia shambani na mundu wa kuvunia, maana mavuno yamekuwa tayari.” |
| BSB 30 Then He asked, “To what can we compare the kingdom of God? With what parable shall we present it? | SWKCV 30 Akawaambia tena, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuueleza? |
| BSB 31 It is like a mustard seed, which is the smallest of all seeds sown upon the earth. | SWKCV 31 Ni kama punje ya haradali, ambayo ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote zinazopandwa ardhini. |
| BSB 32 But after it is planted, it grows to be the largest of all garden plants and puts forth great branches, so that the birds of the air nest in its shade.” | SWKCV 32 Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wanaweza kujenga viota kwenye matawi yake.” |
| BSB 33 With many such parables Jesus spoke the word to them, to the extent that they could understand. | SWKCV 33 Kwa mifano mingine mingi kama hii Yesu alinena nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulielewa. |
| BSB 34 He did not tell them anything without using a parable. But privately He explained everything to His own disciples. | SWKCV 34 Hakusema nao neno lolote pasipo mfano. Lakini alipokuwa na wanafunzi wake, aliwafafanulia kila kitu. |
| BSB 35 When that evening came, He said to His disciples, “Let us cross to the other side.” | SWKCV 35 Siku hiyo ilipokaribia jioni, aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvukeni twende mpaka ngʼambo.” |
| BSB 36 After they had dismissed the crowd, they took Jesus with them, since He was already in the boat. And there were other boats with Him. | SWKCV 36 Wakauacha ule umati wa watu, na wakamchukua vile alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua nyingine nyingi pamoja naye. |
| BSB 37 Soon a violent windstorm came up, and the waves were breaking over the boat, so that it was being swamped. | SWKCV 37 Kukawa na dhoruba kali, nayo mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikawa karibu kujaa maji. |
| BSB 38 But Jesus was in the stern, sleeping on the cushion. So they woke Him and said, “Teacher, don’t You care that we are perishing?” | SWKCV 38 Yesu alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kama tunazama?” |
| BSB 39 Then Jesus got up and rebuked the wind and the sea. “Silence!” He commanded. “Be still!” And the wind died down, and it was perfectly calm. | SWKCV 39 Akaamka, akaukemea ule upepo, akayaambia yale mawimbi, “Uwe kimya! Tulia!” Ule upepo ukatulia, kukawa shwari kabisa. |
| BSB 40 “Why are you so afraid?” He asked. “Do you still have no faith?” | SWKCV 40 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?” |
| BSB 41 Overwhelmed with fear, they asked one another, “Who is this, that even the wind and the sea obey Him?” | SWKCV 41 Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, “Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii?” |
Questions about Mark 4? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.