Mark 3
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Once again Jesus entered the synagogue, and a man with a withered hand was there. | SWKCV 1 Yesu akaingia tena ndani ya sinagogi, na huko palikuwa na mtu aliyepooza mkono. |
| BSB 2 In order to accuse Jesus, they were watching to see if He would heal on the Sabbath. | SWKCV 2 Wakawa wanamwangalia waone kama atamponya siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki. |
| BSB 3 Then Jesus said to the man with the withered hand, “Stand up among us.” | SWKCV 3 Yesu akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Njoo hapa mbele ya watu wote.” |
| BSB 4 And He asked them, “Which is lawful on the Sabbath: to do good or to do evil, to save life or to destroy it?” But they were silent. | SWKCV 4 Kisha Yesu akawauliza, “Je, ni lipi lililo halali siku ya Sabato: Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuua?” Lakini wao wakanyamaza kimya. |
| BSB 5 Jesus looked around at them with anger and sorrow at their hardness of heart. Then He said to the man, “Stretch out your hand.” So he stretched it out, and it was restored. | SWKCV 5 Yesu akawatazama pande zote kwa hasira, akahuzunika sana kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa kabisa! |
| BSB 6 At this, the Pharisees went out and began plotting with the Herodians how they might kill Jesus. | SWKCV 6 Kisha Mafarisayo wakatoka nje, nao wakaanza kufanya shauri la kumuua Yesu wakiwa na Maherode. |
| BSB 7 So Jesus withdrew with His disciples to the sea, accompanied by a large crowd from Galilee, Judea, | SWKCV 7 Yesu pamoja na wanafunzi wake wakaondoka huko wakaenda baharini, nao umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya ukamfuata. |
| BSB 8 Jerusalem, Idumea, the region beyond the Jordan, and the vicinity of Tyre and Sidon. The large crowd came to Him when they heard what great things He was doing. | SWKCV 8 Waliposikia mambo yote aliyokuwa akiyafanya, umati mkubwa wa watu ukamjia kutoka Uyahudi, Yerusalemu, Idumaya, na ngʼambo ya Yordani, pamoja na wale wa sehemu za karibu na Tiro na Sidoni. |
| BSB 9 Jesus asked His disciples to have a boat ready for Him so that the crowd would not crush Him. | SWKCV 9 Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, aliwaambia wanafunzi wake waweke tayari mashua ndogo kwa ajili yake, ili kuwazuia watu kumsonga. |
| BSB 10 For He had healed so many that all who had diseases were pressing forward to touch Him. | SWKCV 10 Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wale wenye magonjwa walikuwa wanasukumana ili wapate kumgusa. |
| BSB 11 And when the unclean spirits saw Him, they fell down before Him and cried out, “You are the Son of God!” | SWKCV 11 Kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kupiga kelele wakisema, “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.” |
| BSB 12 But He warned them sternly not to make Him known. | SWKCV 12 Lakini aliwaonya wasimseme yeye ni nani. |
| BSB 13 Then Jesus went up on the mountain and called for those He wanted, and they came to Him. | SWKCV 13 Yesu akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia. |
| BSB 14 He appointed twelve of them, whom He designated as apostles, to accompany Him, to be sent out to preach, | SWKCV 14 Akawachagua kumi na wawili, ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa pamoja naye, na awatume kwenda kuhubiri |
| BSB 15 and to have authority to drive out demons. | SWKCV 15 na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu. |
| BSB 16 These are the twelve He appointed: Simon (whom He named Peter), | SWKCV 16 Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro); |
| BSB 17 James son of Zebedee and his brother John (whom He named Boanerges, meaning “Sons of Thunder”), | SWKCV 17 Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo); |
| BSB 18 Andrew, Philip, Bartholomew, Matthew, Thomas, James son of Alphaeus, Thaddaeus, Simon the Zealot, | SWKCV 18 Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo, |
| BSB 19 and Judas Iscariot, who betrayed Jesus. | SWKCV 19 na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu. |
| BSB 20 Then Jesus went home, and once again a crowd gathered, so that He and His disciples could not even eat. | SWKCV 20 Kisha Yesu aliporudi nyumbani, umati wa watu ukakusanyika tena, kiasi kwamba yeye na wanafunzi wake hawakuweza kula chakula. |
| BSB 21 When His family heard about this, they went out to take custody of Him, saying, “He is out of His mind.” | SWKCV 21 Ndugu zake walipopata habari wakaja ili kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.” |
| BSB 22 And the scribes who had come down from Jerusalem were saying, “He is possessed by Beelzebul,” and, “By the prince of the demons He drives out demons.” | SWKCV 22 Walimu wa sheria walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli! Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!” |
| BSB 23 So Jesus called them together and began to speak to them in parables: “How can Satan drive out Satan? | SWKCV 23 Basi Yesu akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: “Shetani awezaje kumtoa Shetani? |
| BSB 24 If a kingdom is divided against itself, it cannot stand. | SWKCV 24 Kama ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama. |
| BSB 25 If a house is divided against itself, it cannot stand. | SWKCV 25 Nayo nyumba kama ikigawanyika dhidi yake yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama. |
| BSB 26 And if Satan is divided and rises against himself, he cannot stand; his end has come. | SWKCV 26 Naye Shetani kama akijipinga mwenyewe na awe amegawanyika, hawezi kusimama bali mwisho wake umewadia. |
| BSB 27 Indeed, no one can enter a strong man’s house to steal his possessions unless he first ties up the strong man. Then he can plunder his house. | SWKCV 27 Hakuna mtu yeyote awezaye kuingia kwenye nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu. Ndipo ataweza kuteka nyara mali zake. |
| BSB 28 Truly I tell you, the sons of men will be forgiven all sins and blasphemies, as many as they utter. | SWKCV 28 Amin, nawaambia, dhambi zote na makufuru yote ya wanadamu watasamehewa. |
| BSB 29 But whoever blasphemes against the Holy Spirit will never be forgiven; he is guilty of eternal sin.” | SWKCV 29 Lakini yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.” |
| BSB 30 Jesus made this statement because they were saying, “He has an unclean spirit.” | SWKCV 30 Yesu alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema, “Ana pepo mchafu.” |
| BSB 31 Then Jesus’ mother and brothers came and stood outside. They sent someone in to summon Him, | SWKCV 31 Kisha wakaja ndugu zake Yesu pamoja na mama yake. Wakasimama nje, wakamtuma mtu kumwita. |
| BSB 32 and a crowd was sitting around Him. “Look,” He was told, “Your mother and brothers are outside, asking for You.” | SWKCV 32 Umati wa watu ulikuwa umeketi kumzunguka, nao wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.” |
| BSB 33 But Jesus replied, “Who are My mother and My brothers?” | SWKCV 33 Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni nani?” |
| BSB 34 Looking at those seated in a circle around Him, He said, “Here are My mother and My brothers! | SWKCV 34 Kisha akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka pande zote, akasema, “Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. |
| BSB 35 For whoever does the will of God is My brother and sister and mother.” | SWKCV 35 Mtu yeyote anayetenda mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu na mama yangu.” |
Questions about Mark 3? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.