Proverbs 21
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 The king’s heart is a waterway in the hand of the LORD; He directs it where He pleases. | SWKCV 1 Moyo wa mfalme uko katika mkono wa Bwana; huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo. |
| BSB 2 All a man’s ways seem right to him, but the LORD weighs the heart. | SWKCV 2 Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali Bwana huupima moyo. |
| BSB 3 To do righteousness and justice is more desirable to the LORD than sacrifice. | SWKCV 3 Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu. |
| BSB 4 Haughty eyes and a proud heart—the guides of the wicked—are sin. | SWKCV 4 Macho ya kudharau na moyo wa kiburi, ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi! |
| BSB 5 The plans of the diligent bring plenty, as surely as haste leads to poverty. | SWKCV 5 Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida, kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini. |
| BSB 6 Making a fortune by a lying tongue is a vanishing mist, a deadly pursuit. | SWKCV 6 Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha. |
| BSB 7 The violence of the wicked will sweep them away because they refuse to do what is just. | SWKCV 7 Jeuri ya waovu itawaburuta mbali, kwa kuwa wanakataa kufanya yaliyo sawa. |
| BSB 8 The way of a guilty man is crooked, but the conduct of the innocent is upright. | SWKCV 8 Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu, bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu. |
| BSB 9 Better to live on a corner of the roof than to share a house with a quarrelsome wife. | SWKCV 9 Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi. |
| BSB 10 The soul of the wicked man craves evil; his neighbor finds no favor in his eyes. | SWKCV 10 Mtu mwovu hutamani sana ubaya, jirani yake hapati huruma kutoka kwake. |
| BSB 11 When a mocker is punished, the simple gain wisdom; and when a wise man is instructed, he acquires knowledge. | SWKCV 11 Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa, mjinga hupata hekima; wakati mtu mwenye hekima afundishwapo, hupata maarifa. |
| BSB 12 The Righteous One considers the house of the wicked and brings the wicked to ruin. | SWKCV 12 Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu, naye atawaangamiza waovu. |
| BSB 13 Whoever shuts his ears to the cry of the poor, he too shall cry out and receive no answer. | SWKCV 13 Mtu akiziba masikio asisikie kilio cha maskini, yeye pia atalia, wala hatajibiwa. |
| BSB 14 A gift in secret soothes anger, and a covert bribe pacifies great wrath. | SWKCV 14 Zawadi itolewayo kwa siri hutuliza hasira na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali. |
| BSB 15 Justice executed is a joy to the righteous, but a terror to the workers of iniquity. | SWKCV 15 Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki, bali kitisho kwa watenda mabaya. |
| BSB 16 The man who strays from the path of understanding will rest in the assembly of the dead. | SWKCV 16 Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu, hupumzika katika kundi la waliokufa. |
| BSB 17 He who loves pleasure will become poor; the one who loves wine and oil will never be rich. | SWKCV 17 Mtu apendaye anasa atakuwa maskini, yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri. |
| BSB 18 The wicked become a ransom for the righteous, and the faithless for the upright. | SWKCV 18 Waovu huwa fidia kwa ajili ya wenye haki, nao wasio waaminifu kwa ajili ya wanyofu. |
| BSB 19 Better to live in the desert than with a contentious and ill-tempered wife. | SWKCV 19 Ni afadhali kuishi jangwani kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi. |
| BSB 20 Precious treasures and oil are in the dwelling of the wise, but a foolish man consumes them. | SWKCV 20 Katika nyumba ya mwenye hekima kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta, lakini mtu mpumbavu hutafuna vyote alivyo navyo. |
| BSB 21 He who pursues righteousness and loving devotion finds life, righteousness, and honor. | SWKCV 21 Yeye afuatiaye haki na upendo hupata uzima, mafanikio na heshima. |
| BSB 22 A wise man scales the city of the mighty and pulls down the stronghold in which they trust. | SWKCV 22 Mtu mwenye hekima huushambulia mji wa wenye nguvu, na kuangusha ngome wanazozitegemea. |
| BSB 23 He who guards his mouth and tongue keeps his soul from distress. | SWKCV 23 Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake hujilinda na maafa. |
| BSB 24 Mocker is the name of the proud and arrogant man—of him who acts with excessive pride. | SWKCV 24 Mtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake; hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi. |
| BSB 25 The craving of the slacker kills him because his hands refuse to work. | SWKCV 25 Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake, kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi. |
| BSB 26 All day long he covets more, but the righteous give without restraint. | SWKCV 26 Mchana kutwa hutamani zaidi, lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia. |
| BSB 27 The sacrifice of the wicked is detestable—how much more so when brought with ill intent! | SWKCV 27 Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo, si zaidi sana itolewapo kwa nia mbaya! |
| BSB 28 A lying witness will perish, but the man who listens to truth will speak forever. | SWKCV 28 Shahidi wa uongo ataangamia, bali maneno ya mwenye kusikia yatadumu. |
| BSB 29 A wicked man hardens his face, but the upright man makes his way sure. | SWKCV 29 Mtu mwovu ana uso wa ushupavu, bali mtu mnyofu huzifikiria njia zake. |
| BSB 30 There is no wisdom, no understanding, no counsel that can prevail against the LORD. | SWKCV 30 Hakuna hekima, wala akili, wala mpango unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana. |
| BSB 31 A horse is prepared for the day of battle, but victory is of the LORD. | SWKCV 31 Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, bali ushindi huwa kwa Bwana. |
Questions about Proverbs 21? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.