Psalms 132
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 A song of ascents. O LORD, remember on behalf of David all the hardships he endured, | SWKCV 1 Ee Bwana, mkumbuke Daudi na taabu zote alizozistahimili. |
| BSB 2 how he swore an oath to the LORD, and vowed to the Mighty One of Jacob: | SWKCV 2 Aliapa kiapo kwa Bwana na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo: |
| BSB 3 “I will not enter my house or get into my bed, | SWKCV 3 “Sitaingia nyumbani mwangu au kwenda kitandani mwangu: |
| BSB 4 I will not give sleep to my eyes or slumber to my eyelids, | SWKCV 4 sitaruhusu usingizi katika macho yangu, wala kope zangu kusinzia, |
| BSB 5 until I find a place for the LORD, a dwelling for the Mighty One of Jacob.” | SWKCV 5 mpaka nitakapompatia Bwana mahali, makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.” |
| BSB 6 We heard that the ark was in Ephrathah; we found it in the fields of Jaar. | SWKCV 6 Tulisikia habari hii huko Efrathi, tulikutana nayo katika mashamba ya Yaara: |
| BSB 7 Let us go to His dwelling place; let us worship at His footstool. | SWKCV 7 “Twendeni kwenye makao yake, na tuabudu kwenye kiti cha kuwekea miguu yake; |
| BSB 8 Arise, O LORD, to Your resting place, You and the ark of Your strength. | SWKCV 8 inuka, Ee Bwana, uje mahali pako pa kupumzikia, wewe na Sanduku la nguvu zako. |
| BSB 9 May Your priests be clothed with righteousness, and Your saints shout for joy. | SWKCV 9 Makuhani wako na wavikwe haki, watakatifu wako na waimbe kwa furaha.” |
| BSB 10 For the sake of Your servant David, do not reject Your anointed one. | SWKCV 10 Kwa ajili ya Daudi mtumishi wako, usimkatae mpakwa mafuta wako. |
| BSB 11 The LORD swore an oath to David, a promise He will not revoke: “One of your descendants I will place on your throne. | SWKCV 11 Bwana alimwapia Daudi kiapo, kiapo cha uhakika ambacho hatakitangua: “Nitamweka mmoja wa wazao wako mwenyewe katika kiti chako cha enzi, |
| BSB 12 If your sons keep My covenant and the testimony I will teach them, then their sons will also sit on your throne forever and ever.” | SWKCV 12 kama wanao watashika Agano langu na sheria ninazowafundisha, ndipo wana wao watarithi kiti chako cha enzi milele na milele.” |
| BSB 13 For the LORD has chosen Zion; He has desired it for His home: | SWKCV 13 Kwa maana Bwana ameichagua Sayuni, amepaonea shauku pawe maskani yake: |
| BSB 14 “This is My resting place forever and ever; here I will dwell, for I have desired this home. | SWKCV 14 “Hapa ni mahali pangu pa kupumzika milele na milele; hapa ndipo nitakapoketi nikitawala, kwa sababu nimepaonea shauku: |
| BSB 15 I will bless her with abundant provisions; I will satisfy her poor with bread. | SWKCV 15 Nitambariki kwa kumpa mahitaji tele: nitashibisha maskini wake kwa chakula. |
| BSB 16 I will clothe her priests with salvation, and her saints will sing out in joy. | SWKCV 16 Nitawavika makuhani wake wokovu, nao watakatifu wake watadumu wakiimba kwa furaha. |
| BSB 17 There I will make a horn grow for David; I have prepared a lamp for My anointed one. | SWKCV 17 “Hapa nitamchipushia Daudi pembe, na kuweka taa kwa ajili ya masiya wangu. |
| BSB 18 I will clothe his enemies with shame, but the crown upon him will gleam.” | SWKCV 18 Adui zake nitawavika aibu, bali taji kichwani pake itangʼaa sana.” |
Questions about Psalms 132? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.