Psalms 143
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 A Psalm of David. O LORD, hear my prayer. In Your faithfulness, give ear to my plea; in Your righteousness, answer me. | SWKCV 1 Ee Bwana, sikia sala yangu, sikiliza kilio changu unihurumie; katika uaminifu na haki yako njoo unisaidie. |
| BSB 2 Do not bring Your servant into judgment, for no one alive is righteous before You. | SWKCV 2 Usimhukumu mtumishi wako, kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako. |
| BSB 3 For the enemy has pursued my soul, crushing my life to the ground, making me dwell in darkness like those long since dead. | SWKCV 3 Adui hunifuatilia, hunipondaponda chini; hunifanya niishi gizani kama wale waliokufa zamani. |
| BSB 4 My spirit grows faint within me; my heart is dismayed inside me. | SWKCV 4 Kwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu, moyo wangu ndani yangu unakata tamaa. |
| BSB 5 I remember the days of old; I meditate on all Your works; I consider the work of Your hands. | SWKCV 5 Nakumbuka siku za zamani; natafakari juu ya kazi zako zote, naangalia juu ya kazi ambazo mikono yako imezifanya. |
| BSB 6 I stretch out my hands to You; my soul thirsts for You like a parched land. Selah | SWKCV 6 Nanyoosha mikono yangu kwako, nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame. |
| BSB 7 Answer me quickly, O LORD; my spirit fails. Do not hide Your face from me, or I will be like those who descend to the Pit. | SWKCV 7 Ee Bwana, unijibu haraka, roho yangu inazimia. Usinifiche uso wako, ama sivyo nitafanana na wale washukao shimoni. |
| BSB 8 Let me hear Your loving devotion in the morning, for I have put my trust in You. Teach me the way I should walk, for to You I lift up my soul. | SWKCV 8 Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma, kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako. Nionyeshe njia nitakayoiendea, kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu. |
| BSB 9 Deliver me from my enemies, O LORD; I flee to You for refuge. | SWKCV 9 Ee Bwana, uniokoe na adui zangu, kwa kuwa nimejificha kwako. |
| BSB 10 Teach me to do Your will, for You are my God. May Your good Spirit lead me on level ground. | SWKCV 10 Nifundishe kufanya mapenzi yako, kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu, Roho wako mwema na aniongoze katika nchi tambarare. |
| BSB 11 For the sake of Your name, O LORD, revive me. In Your righteousness, bring my soul out of trouble. | SWKCV 11 Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu, kwa haki yako nitoe katika taabu. |
| BSB 12 And in Your loving devotion, cut off my enemies. Destroy all who afflict me, for I am Your servant. | SWKCV 12 Kwa upendo wako usiokoma, nyamazisha adui zangu; waangamize watesi wangu wote, kwa kuwa mimi ni mtumishi wako. |
Questions about Psalms 143? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.