Psalms 2
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Why do the nations rage and the peoples plot in vain? | SWKCV 1 Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure? |
| BSB 2 The kings of the earth take their stand and the rulers gather together, against the LORD and against His Anointed One: | SWKCV 2 Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. |
| BSB 3 “Let us break Their chains and cast away Their cords.” | SWKCV 3 Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” |
| BSB 4 The One enthroned in heaven laughs; the Lord taunts them. | SWKCV 4 Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. |
| BSB 5 Then He rebukes them in His anger, and terrifies them in His fury: | SWKCV 5 Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, |
| BSB 6 “I have installed My King on Zion, upon My holy mountain.” | SWKCV 6 “Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.” |
| BSB 7 I will proclaim the decree spoken to Me by the LORD: “You are My Son; today I have become Your Father. | SWKCV 7 Nitatangaza amri ya Bwana: Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu, leo mimi nimekuzaa. |
| BSB 8 Ask Me, and I will make the nations Your inheritance, the ends of the earth Your possession. | SWKCV 8 Niombe, nami nitayafanya mataifa kuwa urithi wako, miisho ya dunia kuwa milki yako. |
| BSB 9 You will break them with an iron scepter; You will shatter them like pottery.” | SWKCV 9 Utawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.” |
| BSB 10 Therefore be wise, O kings; be admonished, O judges of the earth. | SWKCV 10 Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima; mwonyeke, enyi watawala wa dunia. |
| BSB 11 Serve the LORD with fear, and rejoice with trembling. | SWKCV 11 Mtumikieni Bwana kwa hofu na mshangilie kwa kutetemeka. |
| BSB 12 Kiss the Son, lest He be angry and you perish in your rebellion, when His wrath ignites in an instant. Blessed are all who take refuge in Him. | SWKCV 12 Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia. |
Questions about Psalms 2? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.