Psalms 38
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 A Psalm of David, for remembrance. O LORD, do not rebuke me in Your anger or discipline me in Your wrath. | SWKCV 1 Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. |
| BSB 2 For Your arrows have pierced me deeply, and Your hand has pressed down on me. | SWKCV 2 Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenishukia. |
| BSB 3 There is no soundness in my body because of Your anger; there is no rest in my bones because of my sin. | SWKCV 3 Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu. |
| BSB 4 For my iniquities have overwhelmed me; they are a burden too heavy to bear. | SWKCV 4 Maovu yangu yamenifunika kama mzigo usiochukulika. |
| BSB 5 My wounds are foul and festering because of my sinful folly. | SWKCV 5 Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu. |
| BSB 6 I am bent and brought low; all day long I go about mourning. | SWKCV 6 Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. |
| BSB 7 For my loins are full of burning pain, and no soundness remains in my body. | SWKCV 7 Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu. |
| BSB 8 I am numb and badly crushed; I groan in anguish of heart. | SWKCV 8 Nimedhoofika na kupondwa kabisa, nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni. |
| BSB 9 O Lord, my every desire is before You; my groaning is not hidden from You. | SWKCV 9 Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako. |
| BSB 10 My heart pounds, my strength fails, and even the light of my eyes has faded. | SWKCV 10 Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia; hata macho yangu yametiwa giza. |
| BSB 11 My beloved and friends shun my disease, and my kinsmen stand at a distance. | SWKCV 11 Rafiki na wenzangu wananikwepa kwa sababu ya majeraha yangu; majirani zangu wanakaa mbali nami. |
| BSB 12 Those who seek my life lay snares; those who wish me harm speak destruction, plotting deceit all day long. | SWKCV 12 Wale wanaotafuta uhai wangu wanatega mitego yao, wale ambao wangetaka kunidhuru huongea juu ya maangamizi yangu; hufanya shauri la hila mchana kutwa. |
| BSB 13 But like a deaf man, I do not hear; and like a mute man, I do not open my mouth. | SWKCV 13 Mimi ni kama mtu kiziwi, asiyeweza kusikia, ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake, |
| BSB 14 I am like a man who cannot hear, whose mouth offers no reply. | SWKCV 14 nimekuwa kama mtu asiyesikia, ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu. |
| BSB 15 I wait for You, O LORD; You will answer, O Lord my God. | SWKCV 15 Ee Bwana, ninakungojea wewe, Ee Bwana Mungu wangu, utajibu. |
| BSB 16 For I said, “Let them not gloat over me—those who taunt me when my foot slips.” | SWKCV 16 Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wasijitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.” |
| BSB 17 For I am ready to fall, and my pain is ever with me. | SWKCV 17 Kwa maana ninakaribia kuanguka, na maumivu yangu yananiandama siku zote. |
| BSB 18 Yes, I confess my iniquity; I am troubled by my sin. | SWKCV 18 Naungama uovu wangu, ninataabishwa na dhambi yangu. |
| BSB 19 Many are my enemies without cause, and many hate me without reason. | SWKCV 19 Wengi ni wale ambao ni adui zangu hodari, wale wanaonichukia bila sababu ni wengi. |
| BSB 20 Those who repay my good with evil attack me for pursuing the good. | SWKCV 20 Wanaolipa maovu kwa wema wangu hunisingizia ninapofuata lililo jema. |
| BSB 21 Do not forsake me, O LORD; be not far from me, O my God. | SWKCV 21 Ee Bwana, usiniache, usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu. |
| BSB 22 Come quickly to help me, O Lord my Savior. | SWKCV 22 Ee Bwana Mwokozi wangu, uje upesi kunisaidia. |
Questions about Psalms 38? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.