Psalms 48
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 A song. A Psalm of the sons of Korah. Great is the LORD, and greatly to be praised in the city of our God, His holy mountain. | SWKCV 1 Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, katika mji wa Mungu wetu, mlima wake mtakatifu. |
| BSB 2 Beautiful in loftiness, the joy of all the earth, like the peaks of Zaphon is Mount Zion, the city of the great King. | SWKCV 2 Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana, furaha ya dunia yote. Kama vilele vya juu sana vya Safoni ni Mlima Sayuni, mji wa Mfalme Mkuu. |
| BSB 3 God is in her citadels; He has shown Himself to be a fortress. | SWKCV 3 Mungu yuko katika ngome zake; amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake. |
| BSB 4 For behold, the kings assembled; they all advanced together. | SWKCV 4 Wakati wafalme walipounganisha nguvu, waliposonga mbele pamoja, |
| BSB 5 They saw and were astounded; they fled in terror. | SWKCV 5 walimwona nao wakashangaa, wakakimbia kwa hofu. |
| BSB 6 Trembling seized them there, anguish like a woman in labor. | SWKCV 6 Kutetemeka kuliwashika huko, maumivu kama ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa. |
| BSB 7 With a wind from the east You wrecked the ships of Tarshish. | SWKCV 7 Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi zilizovunjwa na upepo wa mashariki. |
| BSB 8 As we have heard, so we have seen in the city of the LORD of Hosts, in the city of our God: God will establish her forever. Selah | SWKCV 8 Kama tulivyokuwa tumesikia, ndivyo tulivyoona katika mji wa Bwana Mwenye Nguvu Zote, katika mji wa Mungu wetu: Mungu ataufanya uwe salama milele. |
| BSB 9 Within Your temple, O God, we contemplate Your loving devotion. | SWKCV 9 Ee Mungu, hekaluni mwako tunatafakari upendo wako usiokoma. |
| BSB 10 Your name, O God, like Your praise, reaches to the ends of the earth; Your right hand is full of righteousness. | SWKCV 10 Ee Mungu, kama jina lako lilivyo, sifa zako zinafika hadi miisho ya dunia, mkono wako wa kuume umejazwa na haki. |
| BSB 11 Mount Zion is glad, the daughters of Judah rejoice, on account of Your judgments. | SWKCV 11 Mlima Sayuni unashangilia, vijiji vya Yuda vinafurahi kwa sababu ya hukumu zako. |
| BSB 12 March around Zion, encircle her, count her towers, | SWKCV 12 Tembeeni katika Sayuni, uzungukeni mji, hesabuni minara yake; |
| BSB 13 consider her ramparts, tour her citadels, that you may tell the next generation. | SWKCV 13 yatafakarini vyema maboma yake, angalieni ngome zake, ili mpate kusimulia habari zake kwa kizazi kijacho. |
| BSB 14 For this God is our God forever and ever; He will be our guide even till death. | SWKCV 14 Kwa kuwa huyu Mungu ni Mungu wetu milele na milele; atakuwa kiongozi wetu hata mwisho. |
Questions about Psalms 48? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.