Psalms 50
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 A Psalm of Asaph. The Mighty One, God the LORD, speaks and summons the earth from where the sun rises to where it sets. | SWKCV 1 Mwenye Nguvu, Mungu, Bwana, asema na kuiita dunia, tangu mawio ya jua hadi mahali pake liendapo kutua. |
| BSB 2 From Zion, perfect in beauty, God shines forth. | SWKCV 2 Kutoka Sayuni, penye uzuri mkamilifu, Mungu anaangaza. |
| BSB 3 Our God approaches and will not be silent! Consuming fire precedes Him, and a tempest rages around Him. | SWKCV 3 Mungu wetu anakuja na hatakaa kimya, moto uteketezao unamtangulia, akiwa amezungukwa na tufani kali. |
| BSB 4 He summons the heavens above, and the earth, that He may judge His people: | SWKCV 4 Anaziita mbingu zilizo juu, na nchi, ili aweze kuwahukumu watu wake: |
| BSB 5 “Gather to Me My saints, who made a covenant with Me by sacrifice.” | SWKCV 5 “Nikusanyieni watu wangu waliowekwa wakfu, waliofanya agano nami kwa dhabihu.” |
| BSB 6 And the heavens proclaim His righteousness, for God Himself is Judge. Selah | SWKCV 6 Nazo mbingu zinatangaza haki yake, kwa maana Mungu mwenyewe ni hakimu. |
| BSB 7 “Hear, O My people, and I will speak, O Israel, and I will testify against you: I am God, your God. | SWKCV 7 “Sikieni, enyi watu wangu, nami nitasema, ee Israeli, nami nitashuhudia dhidi yenu: Mimi ndimi Mungu, Mungu wenu. |
| BSB 8 I do not rebuke you for your sacrifices, and your burnt offerings are ever before Me. | SWKCV 8 Sikukemei kwa sababu ya dhabihu zako, au sadaka zako za kuteketezwa, ambazo daima ziko mbele zangu. |
| BSB 9 I have no need for a bull from your stall or goats from your pens, | SWKCV 9 Sina haja ya fahali wa banda lako, au mbuzi wa zizi lako. |
| BSB 10 for every beast of the forest is Mine—the cattle on a thousand hills. | SWKCV 10 Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu. |
| BSB 11 I know every bird in the mountains, and the creatures of the field are Mine. | SWKCV 11 Ninamjua kila ndege mlimani, nao viumbe wa kondeni ni wangu. |
| BSB 12 If I were hungry, I would not tell you, for the world is Mine, and the fullness thereof. | SWKCV 12 Kama ningekuwa na njaa, nisingewaambia ninyi, kwa maana ulimwengu ni wangu, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. |
| BSB 13 Do I eat the flesh of bulls, or drink the blood of goats? | SWKCV 13 Je, mimi hula nyama ya mafahali au kunywa damu ya mbuzi? |
| BSB 14 Sacrifice a thank offering to God, and fulfill your vows to the Most High. | SWKCV 14 Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana, |
| BSB 15 Call upon Me in the day of trouble; I will deliver you, and you will honor Me.” | SWKCV 15 na uniite siku ya taabu; nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.” |
| BSB 16 To the wicked, however, God says, “What right have you to recite My statutes and to bear My covenant on your lips? | SWKCV 16 Lakini kwake mtu mwovu, Mungu asema: “Una haki gani kunena sheria zangu au kuchukua agano langu midomoni mwako? |
| BSB 17 For you hate My instruction and cast My words behind you. | SWKCV 17 Unachukia mafundisho yangu na kuyatupa maneno yangu nyuma yako. |
| BSB 18 When you see a thief, you befriend him, and throw in your lot with adulterers. | SWKCV 18 Unapomwona mwizi, unaungana naye, unapiga kura yako pamoja na wazinzi. |
| BSB 19 You unleash your mouth for evil and harness your tongue to deceit. | SWKCV 19 Unakitumia kinywa chako kwa mabaya na kuuongoza ulimi wako kwa hila. |
| BSB 20 You sit and malign your brother; you slander your own mother’s son. | SWKCV 20 Wanena daima dhidi ya ndugu yako na kumsingizia mwana wa mama yako. |
| BSB 21 You have done these things, and I kept silent; you thought I was just like you. But now I rebuke you and accuse you to your face. | SWKCV 21 Mambo haya unayafanya, nami nimekaa kimya, ukafikiri Mimi nami ni kama wewe. Lakini nitakukemea na kuweka mashtaka mbele yako. |
| BSB 22 Now consider this, you who forget God, lest I tear you to pieces, with no one to rescue you: | SWKCV 22 “Yatafakarini haya, ninyi mnaomsahau Mungu, ama sivyo nitawararua vipande vipande, wala hapatakuwepo na yeyote wa kuwaokoa: |
| BSB 23 He who sacrifices a thank offering honors Me, and to him who rightly orders his way, I will show the salvation of God.” | SWKCV 23 Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi, naye aiandaa njia yake ili nimwonyeshe wokovu wa Mungu.” |
Questions about Psalms 50? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.