Psalms 57
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 For the choirmaster. To the tune of “Do Not Destroy.” A Miktam of David, when he fled from Saul into the cave. Have mercy on me, O God, have mercy, for in You my soul takes refuge. In the shadow of Your wings I will take shelter until the danger has passed. | SWKCV 1 Unihurumie, Ee Mungu, unihurumie, kwa maana nafsi yangu inakukimbilia. Chini ya uvuli wa mbawa zako nitakimbilia mpaka maafa yapite. |
| BSB 2 I cry out to God Most High, to God who fulfills His purpose for me. | SWKCV 2 Namlilia Mungu Aliye Juu Sana, Mungu atimizaye makusudi yake kwangu. |
| BSB 3 He reaches down from heaven and saves me; He rebukes those who trample me. Selah God sends forth His loving devotion and His truth. | SWKCV 3 Hutumana kutoka mbinguni na kuniokoa, akiwakemea wale wanaonifuatilia vikali; Mungu huutuma upendo wake na uaminifu wake. |
| BSB 4 My soul is among the lions; I lie down with ravenous beasts—with men whose teeth are spears and arrows, whose tongues are sharp swords. | SWKCV 4 Niko katikati ya simba, nimelala katikati ya wanyama wenye njaa kuu: watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, ambao ndimi zao ni panga kali. |
| BSB 5 Be exalted, O God, above the heavens; may Your glory cover all the earth. | SWKCV 5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote. |
| BSB 6 They spread a net for my feet; my soul was despondent. They dug a pit before me, but they themselves have fallen into it! Selah | SWKCV 6 Waliitegea miguu yangu nyavu, nikainamishwa chini na dhiki. Wamechimba shimo katika njia yangu, lakini wametumbukia humo wao wenyewe. |
| BSB 7 My heart is steadfast, O God, my heart is steadfast. I will sing and make music. | SWKCV 7 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. |
| BSB 8 Awake, my glory! Awake, O harp and lyre! I will awaken the dawn. | SWKCV 8 Amka, nafsi yangu! Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. |
| BSB 9 I will praise You, O Lord, among the nations; I will sing Your praises among the peoples. | SWKCV 9 Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu. |
| BSB 10 For Your loving devotion reaches to the heavens, and Your faithfulness to the clouds. | SWKCV 10 Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni, uaminifu wako unazifikia anga. |
| BSB 11 Be exalted, O God, above the heavens; may Your glory cover all the earth. | SWKCV 11 Ee Mungu, utukuzwe juu mbinguni, utukufu wako na uwe duniani pote. |
Questions about Psalms 57? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.