Psalms 96
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Sing to the LORD a new song; sing to the LORD, all the earth. | SWKCV 1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya; mwimbieni Bwana dunia yote. |
| BSB 2 Sing to the LORD, bless His name; proclaim His salvation day after day. | SWKCV 2 Mwimbieni Bwana, lisifuni jina lake; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. |
| BSB 3 Declare His glory among the nations, His wonders among all peoples. | SWKCV 3 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. |
| BSB 4 For great is the LORD, and greatly to be praised; He is to be feared above all gods. | SWKCV 4 Kwa kuwa Bwana ni mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. |
| BSB 5 For all the gods of the nations are idols, but it is the LORD who made the heavens. | SWKCV 5 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu. |
| BSB 6 Splendor and majesty are before Him; strength and beauty fill His sanctuary. | SWKCV 6 Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. |
| BSB 7 Ascribe to the LORD, O families of the nations, ascribe to the LORD glory and strength. | SWKCV 7 Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu. |
| BSB 8 Ascribe to the LORD the glory due His name; bring an offering and enter His courts. | SWKCV 8 Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake. |
| BSB 9 Worship the LORD in the splendor of His holiness; tremble before Him, all the earth. | SWKCV 9 Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake. |
| BSB 10 Declare among the nations: “The LORD reigns!” The world is firmly established; it cannot be moved; He will judge the peoples with equity. | SWKCV 10 Katikati ya mataifa semeni, “Bwana anatawala.” Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; atawahukumu watu kwa uadilifu. |
| BSB 11 Let the heavens be glad and the earth rejoice; let the sea resound, and all that fills it. | SWKCV 11 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; |
| BSB 12 Let the fields exult, and all that is in them. Then all the trees of the forest will sing for joy | SWKCV 12 mashamba na yashangilie, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha; |
| BSB 13 before the LORD, for He is coming—He is coming to judge the earth. He will judge the world in righteousness and the peoples in His faithfulness. | SWKCV 13 itaimba mbele za Bwana kwa maana anakuja, anakuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa katika kweli yake. |
Questions about Psalms 96? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.