Romans 10
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Brothers, my heart’s desire and prayer to God for the Israelites is for their salvation. | SWKCV 1 Ndugu zangu, shauku ya moyo wangu na maombi yangu kwa Mungu ni kwa ajili ya Waisraeli, kwamba waokolewe. |
| BSB 2 For I testify about them that they are zealous for God, but not on the basis of knowledge. | SWKCV 2 Kwa maana ninaweza nikashuhudia wazi kwamba wao wana juhudi kubwa kwa ajili ya Mungu, lakini juhudi yao haina maarifa. |
| BSB 3 Because they were ignorant of God’s righteousness and sought to establish their own, they did not submit to God’s righteousness. | SWKCV 3 Kwa kuwa hawakuijua haki itokayo kwa Mungu, wakatafuta kuweka haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. |
| BSB 4 For Christ is the end of the law, to bring righteousness to everyone who believes. | SWKCV 4 Kwa maana Kristo ni ukomo wa sheria ili kuwe na haki kwa kila mtu aaminiye. |
| BSB 5 For concerning the righteousness that is by the law, Moses writes: “The man who does these things will live by them.” | SWKCV 5 Mose anaandika kuhusu haki ile itokanayo na sheria, kwamba, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.” |
| BSB 6 But the righteousness that is by faith says: “Do not say in your heart, ‘Who will ascend into heaven?’ (that is, to bring Christ down) | SWKCV 6 Lakini ile haki itokanayo na imani husema hivi: “Usiseme moyoni mwako, ‘Ni nani atakayepanda mbinguni?’” (yaani ili kumleta Kristo chini) |
| BSB 7 or, ‘Who will descend into the Abyss?’ (that is, to bring Christ up from the dead).” | SWKCV 7 “au ‘Ni nani atashuka kwenda kuzimu?’” (yaani ili kumleta Kristo kutoka kwa wafu.) |
| BSB 8 But what does it say? “The word is near you; it is in your mouth and in your heart,” that is, the word of faith we are proclaiming: | SWKCV 8 Lakini andiko lasemaje? “Lile neno liko karibu nawe, liko kinywani mwako na moyoni mwako,” yaani, lile neno la imani tunalolihubiri. |
| BSB 9 that if you confess with your mouth, “Jesus is Lord,” and believe in your heart that God raised Him from the dead, you will be saved. | SWKCV 9 Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba “Yesu ni Bwana,” na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. |
| BSB 10 For with your heart you believe and are justified, and with your mouth you confess and are saved. | SWKCV 10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu. |
| BSB 11 It is just as the Scripture says: “Anyone who believes in Him will never be put to shame.” | SWKCV 11 Kama yasemavyo Maandiko, “Yeyote amwaminiye hataaibika kamwe.” |
| BSB 12 For there is no difference between Jew and Greek: The same Lord is Lord of all, and gives richly to all who call on Him, | SWKCV 12 Kwa maana hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani, yeye ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao. |
| BSB 13 for, “Everyone who calls on the name of the Lord will be saved.” | SWKCV 13 Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokolewa.” |
| BSB 14 How then can they call on the One in whom they have not believed? And how can they believe in the One of whom they have not heard? And how can they hear without someone to preach? | SWKCV 14 Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? |
| BSB 15 And how can they preach unless they are sent? As it is written: “How beautiful are the feet of those who bring good news!” | SWKCV 15 Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, “Tazama jinsi ilivyo mizuri miguu yao wale wanaohubiri habari njema!” |
| BSB 16 But not all of them welcomed the good news. For Isaiah says, “Lord, who has believed our message?” | SWKCV 16 Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, “Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?” |
| BSB 17 Consequently, faith comes by hearing, and hearing by the word of Christ. | SWKCV 17 Basi, imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. |
| BSB 18 But I ask, did they not hear? Indeed they did: “Their voice has gone out into all the earth, their words to the ends of the world.” | SWKCV 18 Lakini nauliza: Je, wao hawakusikia? Naam, wamesikia, kwa maana: “Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu.” |
| BSB 19 I ask instead, did Israel not understand? First, Moses says: “I will make you jealous by those who are not a nation; I will make you angry by a nation without understanding.” | SWKCV 19 Nami nauliza tena: Je, Waisraeli hawakuelewa? Kwanza, Mose asema, “Nitawafanya mwe na wivu kwa watu wale ambao si taifa. Nitawakasirisha kwa taifa lile lisilo na ufahamu.” |
| BSB 20 And Isaiah boldly says: “I was found by those who did not seek Me; I revealed Myself to those who did not ask for Me.” | SWKCV 20 Naye Isaya kwa ujasiri mwingi anasema, “Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta. Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakunitafuta.” |
| BSB 21 But as for Israel he says: “All day long I have held out My hands to a disobedient and obstinate people.” | SWKCV 21 Lakini kuhusu Israeli anasema, “Mchana kutwa nimewanyooshea watu wakaidi na wasiotii mikono yangu.” |
Questions about Romans 10? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.