Romans 2
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 You, therefore, have no excuse, you who pass judgment on another. For on whatever grounds you judge the other, you are condemning yourself, because you who pass judgment do the same things. | SWKCV 1 Kwa hiyo huna udhuru wowote, wewe utoaye hukumu kwa mwingine, kwa maana katika jambo lolote unalowahukumu wengine, unajihukumu wewe mwenyewe kwa sababu wewe unayehukumu unafanya mambo hayo hayo. |
| BSB 2 And we know that God’s judgment against those who do such things is based on truth. | SWKCV 2 Basi tunajua kwamba hukumu ya Mungu dhidi ya wale wafanyao mambo kama hayo ni ya kweli. |
| BSB 3 So when you, O man, pass judgment on others, yet do the same things, do you think you will escape God’s judgment? | SWKCV 3 Hivyo wewe mwanadamu, utoapo hukumu juu yao na bado unafanya mambo yale yale, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu? |
| BSB 4 Or do you disregard the riches of His kindness, tolerance, and patience, not realizing that God’s kindness leads you to repentance? | SWKCV 4 Au waudharau wingi wa wema, ustahimili na uvumilivu wake, bila kujua kuwa wema wa Mungu wakuelekeza kwenye toba? |
| BSB 5 But because of your hard and unrepentant heart, you are storing up wrath against yourself for the day of wrath, when God’s righteous judgment will be revealed. | SWKCV 5 Lakini kwa sababu ya ukaidi wenu na mioyo yenu isiyotaka kutubu, mnajiwekea akiba ya ghadhabu dhidi yenu wenyewe kwa siku ile ya ghadhabu ya Mungu, wakati hukumu yake ya haki itakapodhihirishwa. |
| BSB 6 God “will repay each one according to his deeds.” | SWKCV 6 Kwa maana Mungu atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake. |
| BSB 7 To those who by perseverance in doing good seek glory, honor, and immortality, He will give eternal life. | SWKCV 7 Wale ambao kwa kuvumilia katika kutenda mema hutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyoharibika, Mungu atawapa uzima wa milele. |
| BSB 8 But for those who are self-seeking and who reject the truth and follow wickedness, there will be wrath and anger. | SWKCV 8 Lakini kwa wale watafutao mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu. |
| BSB 9 There will be trouble and distress for every human being who does evil, first for the Jew, then for the Greek; | SWKCV 9 Kutakuwa na taabu na dhiki kwa kila mmoja atendaye maovu, Myahudi kwanza na mtu wa Mataifa pia, |
| BSB 10 but glory, honor, and peace for everyone who does good, first for the Jew, then for the Greek. | SWKCV 10 bali utukufu, heshima na amani kwa ajili ya kila mmoja atendaye mema, kwa Myahudi kwanza, kisha kwa mtu wa Mataifa. |
| BSB 11 For God does not show favoritism. | SWKCV 11 Kwa maana Mungu hana upendeleo. |
| BSB 12 All who sin apart from the law will also perish apart from the law, and all who sin under the law will be judged by the law. | SWKCV 12 Watu wote waliotenda dhambi pasipo sheria wataangamia pasipo sheria, nao wote wale waliotenda dhambi chini ya sheria watahukumiwa kwa sheria. |
| BSB 13 For it is not the hearers of the law who are righteous before God, but it is the doers of the law who will be declared righteous. | SWKCV 13 Kwa maana si wale wanaoisikia sheria ambao ni wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale wanaoitii sheria ndio watakaohesabiwa haki. |
| BSB 14 Indeed, when Gentiles, who do not have the law, do by nature what the law requires, they are a law to themselves, even though they do not have the law. | SWKCV 14 (Naam, wakati wa watu wa Mataifa, ambao hawana sheria, wanapofanya kwa asili mambo yatakiwayo na sheria, wao ni sheria kwa nafsi zao wenyewe, hata ingawa hawana sheria. |
| BSB 15 So they show that the work of the law is written on their hearts, their consciences also bearing witness, and their thoughts either accusing or defending them | SWKCV 15 Wao wanaonyesha kwamba lile linalotakiwa na sheria limeandikwa kwenye mioyo yao, ambayo pia dhamiri zao zikiwashuhudia, nayo mawazo yao yenye kupingana yatawashtaki au kuwatetea.) |
| BSB 16 on the day when God will judge men’s secrets through Christ Jesus, as proclaimed by my gospel. | SWKCV 16 Hili litatukia siku hiyo Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo, kama isemavyo Injili yangu. |
| BSB 17 Now you, if you call yourself a Jew; if you rely on the law and boast in God; | SWKCV 17 Tazama, wewe ukiwa unaitwa Myahudi na kuitegemea sheria na kujisifia uhusiano wako na Mungu, |
| BSB 18 if you know His will and approve of what is superior because you are instructed by the law; | SWKCV 18 kama unajua mapenzi ya Mungu na kukubali lililo bora kwa sababu umefundishwa na hiyo sheria, |
| BSB 19 if you are convinced that you are a guide for the blind, a light for those in darkness, | SWKCV 19 kama unatambua kuwa wewe ni kiongozi wa vipofu, na mwanga kwa wale walio gizani, |
| BSB 20 an instructor of the foolish, a teacher of infants, because you have in the law the embodiment of knowledge and truth— | SWKCV 20 mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa watoto wachanga, kwa kuwa una maarifa ya kweli katika hiyo sheria, |
| BSB 21 you, then, who teach others, do you not teach yourself? You who preach against stealing, do you steal? | SWKCV 21 basi wewe, uwafundishaye wengine, mbona hujifunzi mwenyewe? Wewe uhubiriye kwamba mtu asiibe, wewe mwenyewe waiba? |
| BSB 22 You who forbid adultery, do you commit adultery? You who abhor idols, do you rob temples? | SWKCV 22 Wewe usemaye mtu asizini, wewe mwenyewe wazini? Wewe uchukiaye miungu ya sanamu, wafanya jambo la kumchukiza katika mahekalu? |
| BSB 23 You who boast in the law, do you dishonor God by breaking the law? | SWKCV 23 Wewe ujivuniaye sheria, wamwaibisha Mungu kwa kuvunja sheria? |
| BSB 24 As it is written: “God’s name is blasphemed among the Gentiles because of you.” | SWKCV 24 Kama ilivyoandikwa, “Kwa ajili yenu ninyi, Jina la Mungu linatukanwa miongoni mwa watu wa Mataifa.” |
| BSB 25 Circumcision has value if you observe the law, but if you break the law, your circumcision has become uncircumcision. | SWKCV 25 Kutahiriwa kuna thamani ikiwa unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa. |
| BSB 26 If a man who is not circumcised keeps the requirements of the law, will not his uncircumcision be regarded as circumcision? | SWKCV 26 Hivyo, ikiwa wale wasiotahiriwa wanatimiza mambo ambayo sheria inataka, je, kutokutahiriwa kwao hakutahesabiwa kuwa sawa na kutahiriwa? |
| BSB 27 The one who is physically uncircumcised yet keeps the law will condemn you who, even though you have the written code and circumcision, are a lawbreaker. | SWKCV 27 Ndipo wale ambao hawakutahiriwa kimwili lakini wanaitii sheria watawahukumu ninyi, ambao ingawa mmetahiriwa na kuijua sana sheria ya Mungu iliyoandikwa, lakini mwaivunja. |
| BSB 28 A man is not a Jew because he is one outwardly, nor is circumcision only outward and physical. | SWKCV 28 Kwa maana mtu si Myahudi kwa vile alivyo kwa nje, wala tohara ya kweli si kitu cha nje au cha kimwili. |
| BSB 29 No, a man is a Jew because he is one inwardly, and circumcision is a matter of the heart, by the Spirit, not by the written code. Such a man’s praise does not come from men, but from God. | SWKCV 29 Lakini mtu ni Myahudi alivyo ndani, nayo tohara ya kweli ni jambo la moyoni, ni la Roho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa namna hiyo hapokei sifa kutoka kwa wanadamu bali kwa Mungu. |
Questions about Romans 2? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.