1 Timothy 2
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 First of all, then, I urge that petitions, prayers, intercessions, and thanksgiving be offered for everyone— | SWKCV 1 Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: |
| BSB 2 for kings and all those in authority—so that we may lead tranquil and quiet lives in all godliness and dignity. | SWKCV 2 kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. |
| BSB 3 This is good and pleasing in the sight of God our Savior, | SWKCV 3 Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu, |
| BSB 4 who wants everyone to be saved and to come to the knowledge of the truth. | SWKCV 4 anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kuijua kweli. |
| BSB 5 For there is one God, and there is one mediator between God and men, the man Christ Jesus, | SWKCV 5 Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu, |
| BSB 6 who gave Himself as a ransom for all—the testimony that was given at just the right time. | SWKCV 6 aliyejitoa mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wanadamu wote: jambo hili lilishuhudiwa kwa wakati wake ufaao. |
| BSB 7 For this reason I was appointed as a preacher, an apostle, and a faithful and true teacher of the Gentiles. I am telling the truth; I am not lying about anything. | SWKCV 7 Nami kwa kusudi hili nimewekwa niwe mhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo wala sisemi uongo), mwalimu wa watu wa Mataifa katika imani na kweli. |
| BSB 8 Therefore I want the men everywhere to pray, lifting up holy hands, without anger or dissension. | SWKCV 8 Nataka kila mahali wanaume wasali wakiinua mikono mitakatifu pasipo hasira wala kugombana. |
| BSB 9 Likewise, I want the women to adorn themselves with respectable apparel, with modesty, and with self-control, not with braided hair or gold or pearls or expensive clothes, | SWKCV 9 Vivyo hivyo nataka wanawake wajipambe kwa adabu na kwa heshima katika mavazi yanayostahili, si kwa kusuka nywele, kuvalia dhahabu, lulu au mavazi ya gharama kubwa, |
| BSB 10 but with good deeds, as is proper for women who profess to worship God. | SWKCV 10 bali kwa matendo mazuri kama iwapasavyo wanawake wanaokiri kuwa wanamcha Mungu. |
| BSB 11 A woman must learn in quietness and full submissiveness. | SWKCV 11 Mwanamke na ajifunze kwa utulivu na kwa utiifu wote. |
| BSB 12 I do not permit a woman to teach or to exercise authority over a man; she is to remain quiet. | SWKCV 12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume. Mwanamke inampasa kukaa kimya. |
| BSB 13 For Adam was formed first, and then Eve. | SWKCV 13 Kwa maana Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva. |
| BSB 14 And it was not Adam who was deceived, but the woman who was deceived and fell into transgression. | SWKCV 14 Wala si Adamu aliyedanganywa, bali ni mwanamke aliyedanganywa akawa mkosaji. |
| BSB 15 Women, however, will be saved through childbearing, if they continue in faith, love, and holiness, with self-control. | SWKCV 15 Lakini mwanamke ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakiendelea kudumu katika imani, upendo na utakatifu, pamoja na kuwa na kiasi. |
Questions about 1 Timothy 2? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.