2 Corinthians 8
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now, brothers, we want you to know about the grace that God has given the churches of Macedonia. | SWKCV 1 Basi sasa ndugu, nataka ninyi mjue kuhusu ile neema ambayo Mungu amewapa makanisa ya Makedonia. |
| BSB 2 In the terrible ordeal they suffered, their abundant joy and deep poverty overflowed into rich generosity. | SWKCV 2 Pamoja na majaribu makali na taabu walizopata, furaha waliyokuwa nayo ilikuwa kubwa, ingawa walikuwa maskini kupindukia, kwa upande wao walifurika kwa wingi wa ukarimu. |
| BSB 3 For I testify that they gave according to their ability and even beyond it. Of their own accord, | SWKCV 3 Kwa maana nashuhudia kwamba wao walitoa kwa kadiri wawezavyo, hata na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe, |
| BSB 4 they earnestly pleaded with us for the privilege of sharing in this service to the saints. | SWKCV 4 wakitusihi kwa bidii wapewe fursa ya kushiriki katika huduma hii ya kuwasaidia watakatifu. |
| BSB 5 And not only did they do as we expected, but they gave themselves first to the Lord and then to us, through the will of God. | SWKCV 5 Wala hawakufanya tulivyotazamia, bali walijitoa wao wenyewe kwa Bwana kwanza na ndipo wakajitoa kwa ajili yetu, kufuatana na mapenzi ya Mungu. |
| BSB 6 So we urged Titus to help complete your act of grace, just as he had started it. | SWKCV 6 Kwa hiyo tulimsihi Tito, kwa kuwa ndiye alianzisha jambo hili, akamilishe tendo hili la neema kwa upande wenu. |
| BSB 7 But just as you excel in everything—in faith, in speech, in knowledge, in complete earnestness, and in the love we inspired in you—see that you also excel in this grace of giving. | SWKCV 7 Lakini kama vile mlivyo mbele sana katika yote: Katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika uaminifu wote na katika upendo wenu kwetu sisi, vivyo hivyo tunataka pia mzidi katika neema hii ya kutoa. |
| BSB 8 I am not giving a command, but I am testing the sincerity of your love through the earnestness of others. | SWKCV 8 Siwaamrishi, lakini nataka kujaribu unyofu wa upendo wenu kwa kuulinganisha na bidii ya wengine. |
| BSB 9 For you know the grace of our Lord Jesus Christ, that though He was rich, yet for your sake He became poor, so that you through His poverty might become rich. | SWKCV 9 Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini wake ninyi mpate kuwa matajiri. |
| BSB 10 And this is my opinion about what is helpful for you in this matter: Last year you were the first not only to give, but even to have such a desire. | SWKCV 10 Ushauri wangu kuhusu lile lililo bora kwenu juu ya jambo hili ni huu: Mwaka uliopita ninyi mlikuwa wa kwanza si tu kutoa lakini pia mlikuwa na shauku ya kufanya hivyo. |
| BSB 11 Now finish the work, so that you may complete it with the same eager desire, according to your means. | SWKCV 11 Sasa ikamilisheni kazi hii kwa shauku kama mlivyoanza, jitoleeni kulingana na uwezo wenu. |
| BSB 12 For if the eagerness is there, the gift is acceptable according to what one has, not according to what he does not have. | SWKCV 12 Kwa kuwa kama nia ya kutoa ipo, kitolewacho kinakubalika kulingana na kile mtu alicho nacho, wala si kwa kile ambacho hana. |
| BSB 13 It is not our intention that others may be relieved while you are burdened, but that there may be equality. | SWKCV 13 Nia yetu si kwamba wengine wasaidike wakati ninyi mnateseka, bali pawe na uwiano. |
| BSB 14 At the present time, your surplus will meet their need, so that in turn their surplus will meet your need. This way there will be equality. | SWKCV 14 Kwa wakati huu, wingi wa vitu mlivyo navyo usaidie kutosheleza mahitaji yao, ili wakati wao watakapokuwa na wingi wa vitu, nao wapate kutosheleza mahitaji yenu. |
| BSB 15 As it is written: “He who gathered much had no excess, and he who gathered little had no shortfall.” | SWKCV 15 Ndipo patakuwa na usawa, kama ilivyoandikwa: “Aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa.” |
| BSB 16 But thanks be to God, who put into the heart of Titus the same devotion I have for you. | SWKCV 16 Ninamshukuru Mungu ambaye amemtia Tito moyo wa kuwajali ninyi kama mimi ninavyowajali. |
| BSB 17 For not only did he welcome our appeal, but he is eagerly coming to you of his own volition. | SWKCV 17 Si kwamba Tito amekubali tu ombi letu, bali anakuja kwenu akiwa na shauku kuliko wakati mwingine, tena kwa hiari yake mwenyewe. |
| BSB 18 Along with Titus we are sending the brother who is praised by all the churches for his work in the gospel. | SWKCV 18 Nasi tunamtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa na makanisa yote kwa huduma yake ya kuhubiri Injili. |
| BSB 19 More than that, this brother was chosen by the churches to accompany us with the gracious offering we administer to honor the Lord Himself and to show our eagerness to help. | SWKCV 19 Zaidi ya hayo, alichaguliwa na makanisa ili asafiri pamoja nasi tulipokuwa tunapeleka matoleo ya ukarimu, kwa ajili ya utukufu wa Bwana mwenyewe, na ili kuonyesha hisani yetu kuwasaidia. |
| BSB 20 We want to avoid any criticism of the way we administer this generous gift. | SWKCV 20 Tunataka kuepuka lawama yoyote kuhusu jinsi tunavyosimamia matoleo haya ya ukarimu. |
| BSB 21 For we are taking great care to do what is right, not only in the eyes of the Lord, but also in the eyes of men. | SWKCV 21 Kwa kuwa tunakusudia kufanya kile kilicho haki si machoni mwa Bwana peke yake, bali pia machoni mwa watu wengine. |
| BSB 22 And we are sending along with them our brother who has proven his earnestness to us many times and in many ways, and now even more so by his great confidence in you. | SWKCV 22 Pamoja nao, tunamtuma ndugu yetu ambaye mara kwa mara ametuthibitishia kwa njia nyingi kwamba ana shauku, naam, zaidi sana sasa kwa sababu analo tumaini kuu kwenu. |
| BSB 23 As for Titus, he is my partner and fellow worker among you. As for our brothers, they are messengers of the churches, the glory of Christ. | SWKCV 23 Kwa habari ya Tito, yeye ni mwenzangu na mtendakazi pamoja nami miongoni mwenu. Kwa habari za ndugu zetu, wao ni wawakilishi wa makanisa, na utukufu kwa Kristo. |
| BSB 24 In full view of the churches, then, show these men the proof of your love and the reason for our boasting about you. | SWKCV 24 Kwa hiyo waonyesheni wazi hawa ndugu uthibitisho wa upendo wenu na sababu inayotufanya tujivune kwa ajili yenu, mbele ya makanisa, ili yapate kuona. |
Questions about 2 Corinthians 8? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.