Job 14
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “Man, who is born of woman, is short of days and full of trouble. | SWKCV 1 “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake ni chache nazo zimejaa taabu. |
| BSB 2 Like a flower, he comes forth, then withers away; like a fleeting shadow, he does not endure. | SWKCV 2 Huchanua kama ua kisha hunyauka; huwa kama kivuli kipitacho upesi, wala hadumu. |
| BSB 3 Do You open Your eyes to one like this? Will You bring him into judgment before You? | SWKCV 3 Je, unamwekea jicho lako mtu kama huyo? Je, utamleta mbele yako katika hukumu? |
| BSB 4 Who can bring out clean from unclean? No one! | SWKCV 4 Ni nani awezaye kutoa kitu safi kutoka kitu najisi? Hakuna awezaye! |
| BSB 5 Since his days are determined and the number of his months is with You, and since You have set limits that he cannot exceed, | SWKCV 5 Siku za mwanadamu zimewekewa mpaka; umekwisha kutangaza idadi ya miezi yake na kuweka mpaka ambao hawezi kuuvuka. |
| BSB 6 look away from him and let him rest, so he can enjoy his day as a hired hand. | SWKCV 6 Hivyo angalia mbali umwache, hadi awe amekamilisha muda wake kama mtu aliyeajiriwa. |
| BSB 7 For there is hope for a tree: If it is cut down, it will sprout again, and its tender shoots will not fail. | SWKCV 7 “Kwa maana lipo tumaini kwa mti; kama ukikatwa utachipuka tena, nayo machipukizi yake mapya hayatakoma. |
| BSB 8 If its roots grow old in the ground and its stump dies in the soil, | SWKCV 8 Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini na kisiki chake kufa udongoni, |
| BSB 9 at the scent of water it will bud and put forth twigs like a sapling. | SWKCV 9 lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua na kutoa machipukizi kama mche. |
| BSB 10 But a man dies and is laid low; he breathes his last, and where is he? | SWKCV 10 Lakini mwanadamu hufa, na huo ndio mwisho wake; hutoa pumzi ya mwisho, naye hayuko tena! |
| BSB 11 As water disappears from the sea and a river becomes parched and dry, | SWKCV 11 Kama vile maji yatowekavyo katika bahari, au mkondo wa mto ukaushwavyo na kuwa mkavu, |
| BSB 12 so a man lies down and does not rise. Until the heavens are no more, he will not be awakened or roused from sleep. | SWKCV 12 ndivyo mwanadamu alalavyo chini asiamke; hadi mbingu zitakapokuwa hazipo tena, wanadamu hawataamka au kuamshwa kutoka kwenye usingizi wao. |
| BSB 13 If only You would hide me in Sheol and conceal me until Your anger has passed! If only You would appoint a time for me and then remember me! | SWKCV 13 “Laiti kama ungenificha kaburini, na kunisitiri hadi hasira yako ipite! Laiti ungeniwekea wakati, na kisha ukanikumbuka! |
| BSB 14 When a man dies, will he live again? All the days of my hard service I will wait, until my renewal comes. | SWKCV 14 Je, kama mtu akifa, aweza kuishi tena? Siku zote za kazi zangu ngumu nitangojea kufanywa upya kwangu. |
| BSB 15 You will call, and I will answer; You will desire the work of Your hands. | SWKCV 15 Utaniita nami nitakuitika; utakionea shauku kiumbe ambacho mikono yako ilikiumba. |
| BSB 16 For then You would count my steps, but would not keep track of my sin. | SWKCV 16 Hakika ndipo utakapozihesabu hatua zangu, lakini hutazifuatia dhambi zangu. |
| BSB 17 My transgression would be sealed in a bag, and You would cover over my iniquity. | SWKCV 17 Makosa yangu yatafungiwa kwa lakiri kwenye mfuko, nawe utazifunika dhambi zangu. |
| BSB 18 But as a mountain erodes and crumbles and a rock is dislodged from its place, | SWKCV 18 “Lakini kama mlima umomonyokavyo na kufikichika na kama vile mwamba uondolewavyo mahali pake, |
| BSB 19 as water wears away the stones and torrents wash away the soil, so You destroy a man’s hope. | SWKCV 19 kama maji yamalizavyo mawe, na mafuriko yachukuavyo udongo, ndivyo unavyoharibu tegemeo la mwanadamu. |
| BSB 20 You forever overpower him, and he passes on; You change his countenance and send him away. | SWKCV 20 Humshinda mara moja kwa daima, naye hutoweka; waibadilisha sura yake na kumwondoa. |
| BSB 21 If his sons receive honor, he does not know it; if they are brought low, he is unaware. | SWKCV 21 Kama wanawe wakipewa heshima, yeye hafahamu; kama wakidharauliwa, yeye haoni. |
| BSB 22 He feels only the pain of his own body and mourns only for himself.” | SWKCV 22 Yeye hasikii kingine isipokuwa maumivu ya mwili wake mwenyewe, naye huomboleza kwa ajili yake mwenyewe.” |
Questions about Job 14? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.