Job 13
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “Indeed, my eyes have seen all this; my ears have heard and understood. | SWKCV 1 “Macho yangu yameona hili lote, masikio yangu yamesikia na kulielewa. |
| BSB 2 What you know, I also know; I am not inferior to you. | SWKCV 2 Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua; mimi si mtu duni kuliko ninyi. |
| BSB 3 Yet I desire to speak to the Almighty and argue my case before God. | SWKCV 3 Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi na kuhojiana shauri langu na Mungu. |
| BSB 4 You, however, smear with lies; you are all worthless physicians. | SWKCV 4 Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo; ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote! |
| BSB 5 If only you would remain silent; for that would be your wisdom! | SWKCV 5 Laiti wote mngenyamaza kimya! Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima. |
| BSB 6 Hear now my argument, and listen to the plea of my lips. | SWKCV 6 Sikieni sasa hoja yangu; sikilizeni kusihi kwangu. |
| BSB 7 Will you speak wickedly on God’s behalf or speak deceitfully for Him? | SWKCV 7 Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu? Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake? |
| BSB 8 Would you show Him partiality or argue in His defense? | SWKCV 8 Mtamwonyesha upendeleo? Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake? |
| BSB 9 Would it be well when He examined you? Could you deceive Him as you would deceive a man? | SWKCV 9 Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi? Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu? |
| BSB 10 Surely He would rebuke you if you secretly showed partiality. | SWKCV 10 Hakika angewakemea kama mkiwapendelea watu kwa siri. |
| BSB 11 Would His majesty not terrify you? Would the dread of Him not fall upon you? | SWKCV 11 Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi? Je, hofu yake isingewaangukia ninyi? |
| BSB 12 Your maxims are proverbs of ashes; your defenses are defenses of clay. | SWKCV 12 Maneno yenu ni mithali za majivu; utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi. |
| BSB 13 Be silent, and I will speak. Then let come to me what may. | SWKCV 13 “Nyamazeni kimya nipate kusema; kisha na yanipate yatakayonipata. |
| BSB 14 Why do I put myself at risk and take my life in my own hands? | SWKCV 14 Kwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu? |
| BSB 15 Though He slay me, I will hope in Him. I will still defend my ways to His face. | SWKCV 15 Ingawa ataniua, bado nitamtumaini; hakika nitazitetea njia zangu mbele zake. |
| BSB 16 Moreover, this will be my salvation, for no godless man can appear before Him. | SWKCV 16 Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu atakayethubutu kuja mbele yake! |
| BSB 17 Listen carefully to my words; let my declaration ring in your ears. | SWKCV 17 Sikilizeni maneno yangu kwa makini; nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho. |
| BSB 18 See now, I have prepared my case; I know that I will be vindicated. | SWKCV 18 Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu, ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki. |
| BSB 19 Can anyone indict me? If so, I will be silent and die. | SWKCV 19 Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu? Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife. |
| BSB 20 Only grant these two things to me, so that I need not hide from You: | SWKCV 20 “Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili, nami sitajificha uso wako: |
| BSB 21 Withdraw Your hand from me, and do not let Your terror frighten me. | SWKCV 21 Ondoa mkono wako uwe mbali nami, nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu. |
| BSB 22 Then call me, and I will answer, or let me speak, and You can reply. | SWKCV 22 Niite kwenye shauri nami nitajibu, au niache niseme, nawe upate kujibu. |
| BSB 23 How many are my iniquities and sins? Reveal to me my transgression and sin. | SWKCV 23 Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda? Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu. |
| BSB 24 Why do You hide Your face and consider me as Your enemy? | SWKCV 24 Kwa nini kuuficha uso wako na kunihesabu mimi kuwa adui yako? |
| BSB 25 Would You frighten a windblown leaf? Would You chase after dry chaff? | SWKCV 25 Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo? Je, utayasaka makapi makavu? |
| BSB 26 For You record bitter accusations against me and bequeath to me the iniquities of my youth. | SWKCV 26 Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu. |
| BSB 27 You put my feet in the stocks and stand watch over all my paths; You set a limit for the soles of my feet. | SWKCV 27 Umeifunga miguu yangu kwenye pingu. Unazichunga kwa makini njia zangu zote kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu. |
| BSB 28 So man wastes away like something rotten, like a moth-eaten garment. | SWKCV 28 “Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza, kama vazi lililoliwa na nondo. |
Questions about Job 13? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.