Job 12
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then Job answered: | SWKCV 1 Ndipo Ayubu akajibu: |
| BSB 2 “Truly then you are the people with whom wisdom itself will die! | SWKCV 2 “Bila shaka ninyi ndio watu, nayo hekima itakoma mtakapokufa! |
| BSB 3 But I also have a mind; I am not inferior to you. Who does not know such things as these? | SWKCV 3 Lakini mimi ninao ufahamu kama ninyi; mimi si duni kwenu. Ni nani asiyejua mambo haya yote? |
| BSB 4 I am a laughingstock to my friends, though I called on God, and He answered. The righteous and upright man is a laughingstock. | SWKCV 4 “Nimekuwa mtu wa kuchekwa na rafiki zangu, ingawa nilimwita Mungu naye akanijibu: mimi ni mtu wa kuchekwa tu, ingawa ni mwadilifu na nisiye na hatia! |
| BSB 5 The one at ease scorns misfortune as the fate of those whose feet are slipping. | SWKCV 5 Wanadamu wakiwa katika utulivu huwa na dharau kwa wale wenye msiba kana kwamba ndiyo haki ya wale ambao miguu yao inateleza. |
| BSB 6 The tents of robbers are safe, and those who provoke God are secure—those who carry their god in their hands. | SWKCV 6 Hema za wanyangʼanyi hazisumbuliwi, wale wanaomghadhibisha Mungu wako salama: wale wamchukuao mungu wao mikononi mwao. |
| BSB 7 But ask the animals, and they will instruct you; ask the birds of the air, and they will tell you. | SWKCV 7 “Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha, au ndege wa angani, nao watawaambia; |
| BSB 8 Or speak to the earth, and it will teach you; let the fish of the sea inform you. | SWKCV 8 au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha, au acheni samaki wa baharini wawape taarifa. |
| BSB 9 Which of all these does not know that the hand of the LORD has done this? | SWKCV 9 Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua kwamba mkono wa Bwana ndio uliofanya hili? |
| BSB 10 The life of every living thing is in His hand, as well as the breath of all mankind. | SWKCV 10 Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe, na pumzi ya wanadamu wote. |
| BSB 11 Does not the ear test words as the tongue tastes its food? | SWKCV 11 Je, sikio haliyajaribu maneno kama vile ulimi uonjavyo chakula? |
| BSB 12 Wisdom is found with the elderly, and understanding comes with long life. | SWKCV 12 Je, hekima haipatikani katikati ya wazee? Je, maisha marefu hayaleti ufahamu? |
| BSB 13 Wisdom and strength belong to God; counsel and understanding are His. | SWKCV 13 “Hekima na nguvu ni vya Mungu; shauri na ufahamu ni vyake yeye. |
| BSB 14 What He tears down cannot be rebuilt; the man He imprisons cannot be released. | SWKCV 14 Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena; mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa. |
| BSB 15 If He holds back the waters, they dry up, and if He releases them, they overwhelm the land. | SWKCV 15 Akizuia maji, huwa pana ukame; akiyaachia maji, huharibu nchi. |
| BSB 16 True wisdom and power belong to Him. The deceived and the deceiver are His. | SWKCV 16 Kwake kuna nguvu na ushindi; adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake. |
| BSB 17 He leads counselors away barefoot and makes fools of judges. | SWKCV 17 Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi. |
| BSB 18 He loosens the bonds placed by kings and fastens a belt around their waists. | SWKCV 18 Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme, na kuwafunga mishipi ya kiunoni. |
| BSB 19 He leads priests away barefoot and overthrows the established. | SWKCV 19 Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu. |
| BSB 20 He deprives the trusted of speech and takes away the discernment of elders. | SWKCV 20 Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika, na kuondoa busara ya wazee. |
| BSB 21 He pours out contempt on nobles and disarms the mighty. | SWKCV 21 Huwamwagia dharau wanaoheshimika, na kuwavua silaha wenye nguvu. |
| BSB 22 He reveals the deep things of darkness and brings deep shadows into light. | SWKCV 22 Hufunua mambo ya ndani ya gizani, na kuyaleta nuruni yale yaliyositirika sana. |
| BSB 23 He makes nations great and destroys them; He enlarges nations, then disperses them. | SWKCV 23 Huyafanya mataifa yatukuke na kuyaangamiza; hufanya mataifa kuwa makubwa, naye huyatawanya. |
| BSB 24 He deprives the earth’s leaders of reason and makes them wander in a trackless wasteland. | SWKCV 24 Huwaondolea viongozi wa nchi akili zao; huwapeleka watangetange nyikani pasipo na njia. |
| BSB 25 They grope in the darkness without light; He makes them stagger like drunkards. | SWKCV 25 Hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga; huwafanya wapepesuke kama walevi. |
Questions about Job 12? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.