Job 24
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “Why does the Almighty not reserve times for judgment? Why may those who know Him never see His days? | SWKCV 1 “Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu? Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio? |
| BSB 2 Men move boundary stones; they pasture stolen flocks. | SWKCV 2 Watu husogeza mawe ya mpaka; huchunga makundi ya wanyama waliyonyangʼanya kwa nguvu. |
| BSB 3 They drive away the donkey of the fatherless and take the widow’s ox in pledge. | SWKCV 3 Huwanyangʼanya yatima punda wao, na kumchukua rehani fahali wa mjane. |
| BSB 4 They push the needy off the road and force all the poor of the land into hiding. | SWKCV 4 Humsukuma mhitaji kutoka njia, na kuwafanya maskini wote wa nchi kulazimika kujificha. |
| BSB 5 Indeed, like wild donkeys in the desert, the poor go to work foraging for food; the wasteland is food for their children. | SWKCV 5 Kama punda-mwitu jangwani, maskini huzunguka katika kazi zao za kutafuta chakula; mahali palipo jangwa huwapa chakula cha watoto wao. |
| BSB 6 They gather fodder in the fields and glean the vineyards of the wicked. | SWKCV 6 Hukusanya chakula mashambani na kuokota masazo katika mashamba ya mizabibu ya waovu. |
| BSB 7 Without clothing, they spend the night naked; they have no covering against the cold. | SWKCV 7 Kwa kukosa nguo, usiku kucha hukaa uchi; hawana chochote cha kujifunika baridi. |
| BSB 8 Drenched by mountain rains, they huddle against the rocks for want of shelter. | SWKCV 8 Hutota kwa mvua za mlimani, nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri. |
| BSB 9 The fatherless infant is snatched from the breast; the nursing child of the poor is seized for a debt. | SWKCV 9 Mtoto yatima hupokonywa matitini; mtoto wachanga wa maskini hunyakuliwa kwa ajili ya deni. |
| BSB 10 Without clothing, they wander about naked. They carry the sheaves, but still go hungry. | SWKCV 10 Kwa kukosa nguo, hutembea uchi; hubeba miganda ya ngano, lakini huwa na njaa. |
| BSB 11 They crush olives within their walls; they tread the winepresses, but go thirsty. | SWKCV 11 Hukamua zeituni katika mawe ya kusagia; hukanyaga mashinikizo, lakini wanaona kiu. |
| BSB 12 From the city, men groan, and the souls of the wounded cry out, yet God charges no one with wrongdoing. | SWKCV 12 Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini, nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada. Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote kwa kutenda mabaya. |
| BSB 13 Then there are those who rebel against the light, not knowing its ways or staying on its paths. | SWKCV 13 “Wako wale wanaoiasi nuru, wasiofahamu njia zake wala hawakai katika mapito yake. |
| BSB 14 When daylight is gone, the murderer rises to kill the poor and needy; in the night he is like a thief. | SWKCV 14 Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka naye huwaua maskini na mhitaji; wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi. |
| BSB 15 The eye of the adulterer watches for twilight. Thinking, ‘No eye will see me,’ he covers his face. | SWKCV 15 Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza, naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’ naye huuficha uso wake. |
| BSB 16 In the dark they dig through houses; by day they shut themselves in, never to experience the light. | SWKCV 16 Katika giza, huvunja majumba, lakini wakati wa mchana hujifungia ndani; hawataki kufanya lolote nuruni. |
| BSB 17 For to them, deep darkness is their morning; surely they are friends with the terrors of darkness! | SWKCV 17 Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao; hujifanya rafiki na vitisho vya gizani. |
| BSB 18 They are but foam on the surface of the water; their portion of the land is cursed, so that no one turns toward their vineyards. | SWKCV 18 “Lakini wao ni povu juu ya maji; sehemu yao juu ya nchi imelaaniwa, hivyo hakuna hata mmoja aendaye kwenye shamba la mizabibu. |
| BSB 19 As drought and heat consume the melting snow, so Sheol steals those who have sinned. | SWKCV 19 Kama vile joto na hari vinyakuavyo theluji iliyoyeyuka, ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo waliotenda dhambi. |
| BSB 20 The womb forgets them; the worm feeds on them; they are remembered no more. So injustice is broken like a tree. | SWKCV 20 Tumbo lililowazaa huwasahau, nao huwa karamu ya mabuu; watu waovu hawakumbukwi tena, lakini huvunjika kama mti. |
| BSB 21 They prey on the barren and childless, and show no kindness to the widow. | SWKCV 21 Huwafanya mawindo wanawake tasa na wasio na watoto, nao hawaonyeshi huruma kwa wajane. |
| BSB 22 Yet by His power, God drags away the mighty; though rising up, they have no assurance of life. | SWKCV 22 Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake; ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha. |
| BSB 23 He gives them a sense of security, but His eyes are on their ways. | SWKCV 23 Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama, lakini macho yake yanaona njia zao. |
| BSB 24 They are exalted for a moment, then they are gone; they are brought low and gathered up like all others; they are cut off like heads of grain. | SWKCV 24 Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka; hushushwa na kukusanywa kama wengine wote, hukatwa kama masuke ya nafaka. |
| BSB 25 If this is not so, then who can prove me a liar and reduce my words to nothing?” | SWKCV 25 “Kama hili sivyo, ni nani awezaye kunithibitisha kuwa mwongo, na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?” |
Questions about Job 24? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.