Job 31
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “I have made a covenant with my eyes. How then could I gaze with desire at a virgin? | SWKCV 1 “Nimefanya agano na macho yangu yasimtazame msichana kwa kumtamani. |
| BSB 2 For what is the allotment of God from above, or the heritage from the Almighty on high? | SWKCV 2 Kwa kuwa fungu la mwanadamu ni gani kutoka kwa Mungu juu, urithi wake kutoka kwa Mungu Mwenye Nguvu Aliye juu? |
| BSB 3 Does not disaster come to the unjust and calamity to the workers of iniquity? | SWKCV 3 Je, si uharibifu kwa watu waovu, maangamizi kwa wale watendao mabaya? |
| BSB 4 Does He not see my ways and count my every step? | SWKCV 4 Je, yeye hazioni njia zangu na kuihesabu kila hatua yangu? |
| BSB 5 If I have walked in falsehood or my foot has rushed to deceit, | SWKCV 5 “Kama nimeishi katika uongo au mguu wangu umekimbilia udanganyifu, |
| BSB 6 let God weigh me with honest scales, that He may know my integrity. | SWKCV 6 Mungu na anipime katika mizani za uaminifu, naye atajua kwamba sina hatia: |
| BSB 7 If my steps have turned from the path, if my heart has followed my eyes, or if impurity has stuck to my hands, | SWKCV 7 kama hatua zangu zimepotoka kutoka kwenye njia, kama moyo wangu umeongozwa na macho yangu, au kama mikono yangu imetiwa unajisi, |
| BSB 8 then may another eat what I have sown, and may my crops be uprooted. | SWKCV 8 basi wengine na wale nilichokipanda, nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe. |
| BSB 9 If my heart has been enticed by my neighbor’s wife, or I have lurked at his door, | SWKCV 9 “Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke, au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu, |
| BSB 10 then may my own wife grind grain for another, and may other men sleep with her. | SWKCV 10 basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine, nao wanaume wengine walale naye. |
| BSB 11 For that would be a heinous crime, an iniquity to be judged. | SWKCV 11 Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu, naam, dhambi ya kuhukumiwa. |
| BSB 12 For it is a fire that burns down to Abaddon; it would root out my entire harvest. | SWKCV 12 Ni moto uwakao kwa Uharibifu; ungekuwa umengʼoa mavuno yangu. |
| BSB 13 If I have rejected the cause of my manservant or maidservant when they made a complaint against me, | SWKCV 13 “Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu, walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu, |
| BSB 14 what will I do when God rises to judge? How will I answer when called to account? | SWKCV 14 nitafanya nini Mungu atakaponikabili? Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu? |
| BSB 15 Did not He who made me in the womb also make them? Did not the same One form us in the womb? | SWKCV 15 Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu, si ndiye aliwaumba? Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote ndani ya mama zetu? |
| BSB 16 If I have denied the desires of the poor or allowed the widow’s eyes to fail, | SWKCV 16 “Ikiwa nimewanyima maskini haja zao, au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike, |
| BSB 17 if I have eaten my morsel alone, not sharing it with the fatherless— | SWKCV 17 kama nimekula chakula changu mwenyewe, bila kuwashirikisha yatima; |
| BSB 18 though from my youth I reared him as would a father, and from my mother’s womb I guided the widow— | SWKCV 18 lakini tangu ujana wangu nimemlea yatima kama ambavyo baba angefanya, nami tangu kuzaliwa kwangu nimewaongoza wajane: |
| BSB 19 if I have seen one perish for lack of clothing, or a needy man without a cloak, | SWKCV 19 kama nilimwona yeyote akiteseka kwa kukosa nguo, au mtu mhitaji asiye na mavazi |
| BSB 20 if his heart has not blessed me for warming him with the fleece of my sheep, | SWKCV 20 ambaye wala moyo wake haukunibariki kwa kumpatia joto kwa mavazi ya manyoya ya kondoo zangu, |
| BSB 21 if I have lifted up my hand against the fatherless because I saw that I had support in the gate, | SWKCV 21 na kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima, nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani, |
| BSB 22 then may my arm fall from my shoulder and be torn from its socket. | SWKCV 22 basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu, nao na uvunjike kutoka kiungio chake. |
| BSB 23 For calamity from God terrifies me, and His splendor I cannot overpower. | SWKCV 23 Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu, nami kwa kuuogopa utukufu wake sikuweza kufanya mambo kama hayo. |
| BSB 24 If I have put my trust in gold or called pure gold my security, | SWKCV 24 “Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu, au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’ |
| BSB 25 if I have rejoiced in my great wealth because my hand had gained so much, | SWKCV 25 kama nimefurahia wingi wa utajiri wangu, ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata, |
| BSB 26 if I have beheld the sun in its radiance or the moon moving in splendor, | SWKCV 26 kama nimelitazama jua katika kungʼaa kwake au mwezi ukienda kwa fahari yake, |
| BSB 27 so that my heart was secretly enticed and my hand threw a kiss from my mouth, | SWKCV 27 hivyo moyo wangu kushawishiwa kwa siri, au kubusu mkono wangu kwa kuviheshimu, |
| BSB 28 this would also be an iniquity to be judged, for I would have denied God on high. | SWKCV 28 basi hiyo pia ingekuwa dhambi ya kuhukumiwa, kwa kuwa ningekuwa si mwaminifu kwa Mungu aishiye juu sana. |
| BSB 29 If I have rejoiced in my enemy’s ruin, or exulted when evil befell him— | SWKCV 29 “Kama nimeshangilia msiba wa adui yangu, au kutazama kwa furaha taabu iliyomjia, |
| BSB 30 I have not allowed my mouth to sin by asking for his life with a curse— | SWKCV 30 lakini sikuruhusu kinywa changu kufanya dhambi kwa kuomba laana dhidi ya maisha yake; |
| BSB 31 if the men of my house have not said, ‘Who is there who has not had his fill?’— | SWKCV 31 kama watu wa nyumbani mwangu kamwe hawakusema, ‘Ni nani ambaye hajashibishwa na nyama ya Ayubu?’ |
| BSB 32 but no stranger had to lodge on the street, for my door has been open to the traveler— | SWKCV 32 Lakini hakuna mgeni aliyelala njiani, kwa maana mlango wangu ulikuwa wazi kwa msafiri; |
| BSB 33 if I have covered my transgressions like Adam by hiding my guilt in my heart, | SWKCV 33 kama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo, kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu, |
| BSB 34 because I greatly feared the crowds and the contempt of the clans terrified me, so that I kept silent and would not go outside— | SWKCV 34 kwa sababu ya kuogopa umati wa watu, na hivyo kuwa na hofu ya kudharauliwa na jamaa, nikanyamaza kimya nisitoke nje ya mlango: |
| BSB 35 (Oh, that I had one to hear me! Here is my signature. Let the Almighty answer me; let my accuser compose an indictment. | SWKCV 35 (“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia! Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu: Mwenyezi na anijibu; mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi. |
| BSB 36 Surely I would carry it on my shoulder and wear it like a crown. | SWKCV 36 Hakika ningeyavaa begani mwangu, ningeyavaa kama taji. |
| BSB 37 I would give account of all my steps; I would approach Him like a prince.)— | SWKCV 37 Ningempa hesabu ya kila hatua yangu, ningemwendea kama mwana wa mfalme.) |
| BSB 38 if my land cries out against me and its furrows weep together, | SWKCV 38 “Kama nchi yangu inalia dhidi yangu, na mifereji yake yote imelowana kwa machozi, |
| BSB 39 if I have devoured its produce without payment or broken the spirit of its tenants, | SWKCV 39 kama nimekula mazao yake bila malipo, au kuvunja mioyo ya wapangaji wake, |
| BSB 40 then let briers grow instead of wheat and stinkweed instead of barley.” Thus conclude the words of Job. | SWKCV 40 basi miiba na iote badala ya ngano, na magugu badala ya shayiri.” Mwisho wa maneno ya Ayubu. |
Questions about Job 31? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.