Job 30
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “But now they mock me, men younger than I am, whose fathers I would have refused to put with my sheep dogs. | SWKCV 1 “Lakini sasa watu wadogo kwa umri kuniliko wananidhihaki, watu ambao baba zao ningekataa kwa dharau kuwaweka pamoja na mbwa wangu wa kulinda kondoo. |
| BSB 2 What use to me was the strength of their hands, since their vigor had left them? | SWKCV 2 Nguvu za mikono yao zingekuwa na faida gani kwangu, kwa kuwa nguvu zao zilikuwa zimewaishia? |
| BSB 3 Gaunt from poverty and hunger, they gnawed the dry land, and the desolate wasteland by night. | SWKCV 3 Wakiwa wamekonda kutokana na kupungukiwa na kwa njaa, walizurura usiku katika nchi kame iliyo ukiwa. |
| BSB 4 They plucked mallow among the shrubs, and the roots of the broom tree were their food. | SWKCV 4 Katika vichaka walikusanya mimea ya chumvi, nacho chakula chao kilikuwa mizizi ya mti wa mfagio. |
| BSB 5 They were banished from among men, shouted at like thieves, | SWKCV 5 Walifukuzwa mbali na watu wao, wakipigiwa kelele kama wevi. |
| BSB 6 so that they lived on the slopes of the wadis, among the rocks and in holes in the ground. | SWKCV 6 Walilazimika kuishi katika mikondo ya vijito vilivyokauka, kwenye majabali na mahandaki. |
| BSB 7 They cried out among the shrubs and huddled beneath the nettles. | SWKCV 7 Kwenye vichaka walilia kama punda, na walijisongasonga pamoja kwenye vichaka. |
| BSB 8 A senseless and nameless brood, they were driven off the land. | SWKCV 8 Wao ni watoto wa wapumbavu wenye asili ya ubaya, waliofukuzwa watoke katika nchi. |
| BSB 9 And now they mock me in song; I have become a byword among them. | SWKCV 9 “Nao sasa wana wao wananidhihaki katika nyimbo; nimekuwa kitu cha dhihaka kwao. |
| BSB 10 They abhor me and keep far from me; they do not hesitate to spit in my face. | SWKCV 10 Wananichukia sana na kujitenga nami, wala hawasiti kunitemea mate usoni. |
| BSB 11 Because God has unstrung my bow and afflicted me, they have cast off restraint in my presence. | SWKCV 11 Sasa kwa kuwa Mungu ameilegeza kamba ya upinde wangu na kunitesa, wamekuwa huru kunitendea waonavyo. |
| BSB 12 The rabble arises at my right; they lay snares for my feet and build siege ramps against me. | SWKCV 12 Kuume kwangu kundi linashambulia; wao huitegea miguu yangu tanzi, na kunizingira. |
| BSB 13 They tear up my path; they profit from my destruction, with no one to restrain them. | SWKCV 13 Huizuia njia yangu, nao hufanikiwa katika kuniletea maafa, nami sina yeyote wa kunisaidia. |
| BSB 14 They advance as through a wide breach; through the ruins they keep rolling in. | SWKCV 14 Wananijia kama watu wapitao katika ufa mpana; katikati ya magofu huja na kunishambulia. |
| BSB 15 Terrors are turned loose against me; they drive away my dignity as by the wind, and my prosperity has passed like a cloud. | SWKCV 15 Vitisho vimenifunika; heshima yangu imetoweshwa kama kwa upepo, salama yangu imetoweka kama wingu. |
| BSB 16 And now my soul is poured out within me; days of affliction grip me. | SWKCV 16 “Sasa maisha yangu yamefikia mwisho; siku za mateso zimenikamata. |
| BSB 17 Night pierces my bones, and my gnawing pains never rest. | SWKCV 17 Usiku mifupa yangu inachoma; maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe. |
| BSB 18 With great force He grasps my garment; He seizes me by the collar of my tunic. | SWKCV 18 Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo; hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu. |
| BSB 19 He throws me into the mud, and I have become like dust and ashes. | SWKCV 19 Yeye amenitupa kwenye matope, nami nimekuwa kama mavumbi na majivu. |
| BSB 20 I cry out to You for help, but You do not answer; when I stand up, You merely look at me. | SWKCV 20 “Ee Bwana, ninakulilia wewe lakini hunijibu; ninasimama, nawe unanitazama tu. |
| BSB 21 You have ruthlessly turned on me; You oppose me with Your strong hand. | SWKCV 21 Wewe unanigeukia bila huruma; unanishambulia kwa nguvu za mkono wako. |
| BSB 22 You snatch me up into the wind and drive me before it; You toss me about in the storm. | SWKCV 22 Unaninyakua na kunipeperusha kwa upepo; umenirusha huku na huko kwenye dhoruba kali. |
| BSB 23 Yes, I know that You will bring me down to death, to the place appointed for all the living. | SWKCV 23 Ninajua utanileta mpaka kifoni, mahali ambapo wenye uhai wote wamewekewa. |
| BSB 24 Yet no one stretches out his hand against a ruined man when he cries for help in his distress. | SWKCV 24 “Hakika hakuna yeyote amshambuliaye mhitaji, anapoomba msaada katika shida yake. |
| BSB 25 Have I not wept for those in trouble? Has my soul not grieved for the needy? | SWKCV 25 Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini? |
| BSB 26 But when I hoped for good, evil came; when I looked for light, darkness fell. | SWKCV 26 Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja. |
| BSB 27 I am churning within and cannot rest; days of affliction confront me. | SWKCV 27 Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili. |
| BSB 28 I go about blackened, but not by the sun. I stand up in the assembly and cry for help. | SWKCV 28 Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada. |
| BSB 29 I have become a brother of jackals, a companion of ostriches. | SWKCV 29 Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi. |
| BSB 30 My skin grows black and peels, and my bones burn with fever. | SWKCV 30 Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika; mifupa yangu inaungua kwa homa. |
| BSB 31 My harp is tuned to mourning and my flute to the sound of weeping. | SWKCV 31 Kinubi changu kimegeuka kuwa maombolezo, nayo filimbi yangu imekuwa sauti ya kilio. |
Questions about Job 30? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.