Luke 1
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Many have undertaken to compose an account of the things that have been fulfilled among us, | SWKCV 1 Kwa kuwa watu wengi wamekaa ili kuandika habari za mambo yaliyotukia katikati yetu, |
| BSB 2 just as they were handed down to us by the initial eyewitnesses and servants of the word. | SWKCV 2 kama vile yalivyokabidhiwa kwetu na wale waliokuwa mashahidi walioyaona na watumishi wa Bwana, |
| BSB 3 Therefore, having carefully investigated everything from the beginning, it seemed good also to me to write an orderly account for you, most excellent Theophilus, | SWKCV 3 mimi nami baada ya kuchunguza kila kitu kwa uangalifu kuanzia mwanzo, niliamua kukuandikia habari za mambo hayo, ewe mtukufu Theofilo, |
| BSB 4 so that you may know the certainty of the things you have been taught. | SWKCV 4 ili upate kujua ukweli kuhusu yale uliyofundishwa. |
| BSB 5 In the time of Herod king of Judea there was a priest named Zechariah, who belonged to the priestly division of Abijah, and whose wife Elizabeth was a descendant of Aaron. | SWKCV 5 Wakati wa Herode mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zekaria, ambaye alikuwa wa ukoo wa kikuhani wa Abiya. Elizabeti mkewe alikuwa pia mzao wa Aroni. |
| BSB 6 Both of them were righteous in the sight of God, walking blamelessly in all the commandments and decrees of the Lord. | SWKCV 6 Zekaria na Elizabeti mkewe wote walikuwa watu wanyofu mbele za Mungu, wakizishika amri zote za Bwana na maagizo yote bila lawama. |
| BSB 7 But they had no children, because Elizabeth was barren, and they were both well along in years. | SWKCV 7 Lakini walikuwa hawana watoto, kwa sababu Elizabeti alikuwa tasa; nao wote wawili walikuwa wazee sana. |
| BSB 8 One day while Zechariah’s division was on duty and he was serving as priest before God, | SWKCV 8 Siku moja ilipokuwa zamu ya kikundi cha Zekaria, yeye akifanya kazi ya ukuhani Hekaluni mbele za Mungu, |
| BSB 9 he was chosen by lot, according to the custom of the priesthood, to enter the temple of the Lord and burn incense. | SWKCV 9 alichaguliwa kwa kura kwa kufuata desturi za ukuhani, kuingia Hekaluni mwa Bwana ili kufukiza uvumba. |
| BSB 10 And at the hour of the incense offering, the whole congregation was praying outside. | SWKCV 10 Nao wakati wa kufukiza uvumba ulipowadia, wale wote waliokuwa wamekusanyika ili kuabudu walikuwa nje wakiomba. |
| BSB 11 Just then an angel of the Lord appeared to Zechariah, standing at the right side of the altar of incense. | SWKCV 11 Ndipo malaika wa Bwana, akiwa amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia uvumba, akamtokea Zekaria. |
| BSB 12 When Zechariah saw him, he was startled and gripped with fear. | SWKCV 12 Zekaria alipomwona huyo malaika, akafadhaika sana, akajawa na hofu. |
| BSB 13 But the angel said to him, “Do not be afraid, Zechariah, because your prayer has been heard. Your wife Elizabeth will bear you a son, and you are to give him the name John. | SWKCV 13 Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zekaria, kwa maana Mungu amesikia maombi yako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yohana. |
| BSB 14 He will be a joy and delight to you, and many will rejoice at his birth, | SWKCV 14 Yeye atakuwa furaha na shangwe kwako, nao watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake. |
| BSB 15 for he will be great in the sight of the Lord. He shall never take wine or strong drink, and he will be filled with the Holy Spirit even from his mother’s womb. | SWKCV 15 Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele za Bwana, kamwe hataonja mvinyo wala kinywaji chochote cha kulevya, naye atajazwa Roho Mtakatifu hata kabla ya kuzaliwa kwake. |
| BSB 16 Many of the sons of Israel he will turn back to the Lord their God. | SWKCV 16 Naye atawageuza wengi wa wana wa Israeli warudi kwa Bwana Mungu wao. |
| BSB 17 And he will go on before the Lord in the spirit and power of Elijah, to turn the hearts of the fathers to their children and the disobedient to the wisdom of the righteous—to make ready a people prepared for the Lord.” | SWKCV 17 Naye atatangulia mbele za Bwana katika roho na nguvu ya Eliya, ili kuigeuza mioyo ya baba kuwaelekea watoto wao, na wasiotii warejee katika hekima ya wenye haki, ili kuliweka tayari taifa lililoandaliwa kwa ajili ya Bwana.” |
| BSB 18 “How can I be sure of this?” Zechariah asked the angel. “I am an old man, and my wife is well along in years.” | SWKCV 18 Zekaria akamuuliza malaika, “Jambo hilo linawezekanaje? Mimi ni mzee na mke wangu pia ana umri mkubwa.” |
| BSB 19 “I am Gabriel,” replied the angel. “I stand in the presence of God, and I have been sent to speak to you and to bring you this good news. | SWKCV 19 Malaika akamjibu, akamwambia, “Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu, nami nimetumwa kwako ili nikuambie habari hizi njema. |
| BSB 20 And now you will be silent and unable to speak until the day this comes to pass, because you did not believe my words, which will be fulfilled at their proper time.” | SWKCV 20 Basi sasa kwa kuwa hujaamini maneno yangu ambayo yatatimizwa kwa wakati wake, utakuwa bubu hadi siku ile mambo haya yatakapotukia.” |
| BSB 21 Meanwhile, the people were waiting for Zechariah and wondering why he took so long in the temple. | SWKCV 21 Wakati huo watu walikuwa wanamngojea Zekaria nje huku wakishangaa kukawia kwake mle Hekaluni. |
| BSB 22 When he came out and was unable to speak to them, they realized he had seen a vision in the temple. He kept making signs to them but remained unable to speak. | SWKCV 22 Alipotoka akawa hawezi kusema nao, wao wakatambua kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Lakini kwa kuwa alikuwa bubu, akawa anawaashiria kwa mikono. |
| BSB 23 And when the days of his service were complete, he returned home. | SWKCV 23 Muda wake wa kuhudumu Hekaluni ulipomalizika, akarudi nyumbani kwake. |
| BSB 24 After these days, his wife Elizabeth became pregnant and for five months remained in seclusion. She declared, | SWKCV 24 Baada ya muda usio mrefu, Elizabeti mkewe akapata mimba, naye akajitenga kwa miezi mitano. |
| BSB 25 “The Lord has done this for me. In these days He has shown me favor and taken away my disgrace among the people.” | SWKCV 25 Akasema, “Hili ndilo Bwana alilonitendea aliponiangalia kwa upendeleo na kuniondolea aibu yangu mbele ya watu.” |
| BSB 26 In the sixth month, God sent the angel Gabriel to a town in Galilee called Nazareth, | SWKCV 26 Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Gabrieli aende Galilaya katika mji wa Nazareti, |
| BSB 27 to a virgin pledged in marriage to a man named Joseph, who was of the house of David. And the virgin’s name was Mary. | SWKCV 27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yosefu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Maria. |
| BSB 28 The angel appeared to her and said, “Greetings, you who are highly favored! The Lord is with you.” | SWKCV 28 Naye malaika akaja kwake akamwambia: “Salamu, wewe uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!” |
| BSB 29 Mary was greatly troubled at his words and wondered what kind of greeting this might be. | SWKCV 29 Maria akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, “Salamu hii ni ya namna gani?” |
| BSB 30 So the angel told her, “Do not be afraid, Mary, for you have found favor with God. | SWKCV 30 Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Maria, umepata kibali kwa Mungu. |
| BSB 31 Behold, you will conceive and give birth to a son, and you are to give Him the name Jesus. | SWKCV 31 Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanaume na utamwita jina lake Yesu. |
| BSB 32 He will be great and will be called the Son of the Most High. The Lord God will give Him the throne of His father David, | SWKCV 32 Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. |
| BSB 33 and He will reign over the house of Jacob forever. His kingdom will never end!” | SWKCV 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” |
| BSB 34 “How can this be,” Mary asked the angel, “since I am a virgin?” | SWKCV 34 Maria akamuuliza huyo malaika, “Maadamu mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?” |
| BSB 35 The angel replied, “The Holy Spirit will come upon you, and the power of the Most High will overshadow you. So the Holy One to be born will be called the Son of God. | SWKCV 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli. Kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu. |
| BSB 36 Look, even Elizabeth your relative has conceived a son in her old age, and she who was called barren is in her sixth month. | SWKCV 36 Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake, na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. |
| BSB 37 For no word from God will ever fail.” | SWKCV 37 Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.” |
| BSB 38 “I am the Lord’s servant,” Mary answered. “May it happen to me according to your word.” Then the angel left her. | SWKCV 38 Maria akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka, akamwacha. |
| BSB 39 In those days Mary got ready and hurried to a town in the hill country of Judah, | SWKCV 39 Wakati huo Maria akajiandaa, akaharakisha kwenda katika mji mmoja kwenye vilima vya Uyahudi. |
| BSB 40 where she entered the home of Zechariah and greeted Elizabeth. | SWKCV 40 Akaingia nyumbani kwa Zekaria na kumsalimu Elizabeti. |
| BSB 41 When Elizabeth heard Mary’s greeting, the baby leaped in her womb, and Elizabeth was filled with the Holy Spirit. | SWKCV 41 Naye Elizabeti aliposikia salamu ya Maria, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, |
| BSB 42 In a loud voice she exclaimed, “Blessed are you among women, and blessed is the fruit of your womb! | SWKCV 42 akapaza sauti kwa nguvu akasema, “Umebarikiwa wewe miongoni mwa wanawake, naye mtoto utakayemzaa amebarikiwa. |
| BSB 43 And why am I so honored, that the mother of my Lord should come to me? | SWKCV 43 Lakini ni kwa nini mimi nimepata upendeleo kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? |
| BSB 44 For as soon as the sound of your greeting reached my ears, the baby in my womb leaped for joy. | SWKCV 44 Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliyeko tumboni mwangu aliruka kwa furaha. |
| BSB 45 Blessed is she who has believed that the Lord’s word to her will be fulfilled.” | SWKCV 45 Amebarikiwa yeye aliyeamini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa.” |
| BSB 46 Then Mary said: “My soul magnifies the Lord, | SWKCV 46 Naye Maria akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, |
| BSB 47 and my spirit rejoices in God my Savior! | SWKCV 47 nayo roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu, |
| BSB 48 For He has looked with favor on the humble state of His servant. From now on all generations will call me blessed. | SWKCV 48 kwa kuwa ameangalia kwa fadhili unyonge wa mtumishi wake. Hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita aliyebarikiwa, |
| BSB 49 For the Mighty One has done great things for me. Holy is His name. | SWKCV 49 kwa maana yeye Mwenye Nguvu amenitendea mambo ya ajabu: jina lake ni takatifu. |
| BSB 50 His mercy extends to those who fear Him, from generation to generation. | SWKCV 50 Rehema zake huwaendea wale wamchao, kutoka kizazi hadi kizazi. |
| BSB 51 He has performed mighty deeds with His arm; He has scattered those who are proud in the thoughts of their hearts. | SWKCV 51 Kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu kwa mkono wake; amewatawanya wale wenye kiburi ndani ya mioyo yao. |
| BSB 52 He has brought down rulers from their thrones, but has exalted the humble. | SWKCV 52 Amewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya enzi, lakini amewainua wanyenyekevu. |
| BSB 53 He has filled the hungry with good things, but has sent the rich away empty. | SWKCV 53 Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu. |
| BSB 54 He has helped His servant Israel, remembering to be merciful, | SWKCV 54 Amemsaidia mtumishi wake Israeli, kwa kukumbuka ahadi yake ya kumrehemu |
| BSB 55 as He promised to our fathers, to Abraham and his descendants forever.” | SWKCV 55 Abrahamu na uzao wake milele, kama alivyowaahidi baba zetu.” |
| BSB 56 Mary stayed with Elizabeth for about three months and then returned home. | SWKCV 56 Maria akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyumbani kwake. |
| BSB 57 When the time came for Elizabeth to have her child, she gave birth to a son. | SWKCV 57 Ulipowadia wakati wa Elizabeti kujifungua, alizaa mtoto mwanaume. |
| BSB 58 Her neighbors and relatives heard that the Lord had shown her great mercy, and they rejoiced with her. | SWKCV 58 Majirani zake na jamii zake wakasikia jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu, nao wakafurahi pamoja naye. |
| BSB 59 On the eighth day, when they came to circumcise the child, they were going to name him after his father Zechariah. | SWKCV 59 Siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka yule mtoto aitwe Zekaria, ambalo ndilo jina la baba yake. |
| BSB 60 But his mother replied, “No! He shall be called John.” | SWKCV 60 Lakini mama yake akakataa na kusema, “Hapana! Jina lake ataitwa Yohana.” |
| BSB 61 They said to her, “There is no one among your relatives who bears this name.” | SWKCV 61 Wakamwambia, “Hakuna mtu yeyote katika jamaa yako mwenye jina kama hilo.” |
| BSB 62 So they made signs to his father to find out what he wanted to name the child. | SWKCV 62 Basi wakamfanyia Zekaria baba yake ishara ili kujua kwamba yeye angependa kumpa mtoto jina gani. |
| BSB 63 Zechariah asked for a tablet and wrote, “His name is John.” And they were all amazed. | SWKCV 63 Akaomba wampe kibao cha kuandikia na kwa mshangao wa kila mtu akaandika: “Jina lake ni Yohana.” |
| BSB 64 Immediately Zechariah’s mouth was opened and his tongue was released, and he began to speak, praising God. | SWKCV 64 Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake ukaachiwa, akawa anaongea akimsifu Mungu. |
| BSB 65 All their neighbors were filled with awe, and people throughout the hill country of Judea were talking about these events. | SWKCV 65 Majirani wote wakajawa na hofu ya Mungu, na katika nchi yote ya vilima vya Uyahudi watu walikuwa wakinena juu ya mambo haya yote. |
| BSB 66 And all who heard this wondered in their hearts and asked, “What then will this child become?” For the Lord’s hand was with him. | SWKCV 66 Kila aliyesikia habari hizi alishangaa akauliza, “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye. |
| BSB 67 Then his father Zechariah was filled with the Holy Spirit and prophesied: | SWKCV 67 Zekaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akatoa unabii, akisema: |
| BSB 68 “Blessed be the Lord, the God of Israel, because He has visited and redeemed His people. | SWKCV 68 “Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa. |
| BSB 69 He has raised up a horn of salvation for us in the house of His servant David, | SWKCV 69 Naye ametusimamishia pembe ya wokovu katika nyumba ya Daudi mtumishi wake, |
| BSB 70 as He spoke through His holy prophets, those of ages past, | SWKCV 70 kama alivyonena kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani, |
| BSB 71 salvation from our enemies and from the hand of all who hate us, | SWKCV 71 kwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu, na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao: |
| BSB 72 to show mercy to our fathers and to remember His holy covenant, | SWKCV 72 ili kuonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka Agano lake takatifu, |
| BSB 73 the oath He swore to our father Abraham, to grant us | SWKCV 73 kiapo alichomwapia baba yetu Abrahamu: |
| BSB 74 deliverance from hostile hands, that we may serve Him without fear, | SWKCV 74 kutuokoa kutoka mikononi mwa adui zetu, tupate kumtumikia yeye pasipo hofu |
| BSB 75 in holiness and righteousness before Him all the days of our lives. | SWKCV 75 katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote. |
| BSB 76 And you, child, will be called a prophet of the Most High; for you will go on before the Lord to prepare the way for Him, | SWKCV 76 “Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana; kwa kuwa utamtangulia Bwana na kuandaa njia kwa ajili yake, |
| BSB 77 to give to His people the knowledge of salvation through the forgiveness of their sins, | SWKCV 77 kuwajulisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao, |
| BSB 78 because of the tender mercy of our God, by which the Dawn will visit us from on high, | SWKCV 78 kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu, nuru itokayo juu itatuzukia |
| BSB 79 to shine on those who live in darkness and in the shadow of death, to guide our feet into the path of peace.” | SWKCV 79 ili kuwaangazia wale waishio gizani na katika uvuli wa mauti, kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.” |
| BSB 80 And the child grew and became strong in spirit; and he lived in the wilderness until the time of his public appearance to Israel. | SWKCV 80 Yule mtoto akakua na kuongezeka nguvu katika roho; akaishi nyikani hadi siku ile alipojionyesha hadharani kwa Waisraeli. |
Questions about Luke 1? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.