Luke 19
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then Jesus entered Jericho and was passing through. | SWKCV 1 Yesu akaingia Yeriko, naye alikuwa anapita katikati ya huo mji. |
| BSB 2 And there was a man named Zacchaeus, a chief tax collector, who was very wealthy. | SWKCV 2 Tazama, palikuwa na mtu mmoja mkuu wa watoza ushuru naye alikuwa tajiri, jina lake Zakayo. |
| BSB 3 He was trying to see who Jesus was, but could not see over the crowd because he was small in stature. | SWKCV 3 Yeye alikuwa akijitahidi kumwona Yesu ni mtu wa namna gani. Lakini kutokana na umati mkubwa wa watu hakuweza kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo. |
| BSB 4 So he ran on ahead and climbed a sycamore tree to see Him, since Jesus was about to pass that way. | SWKCV 4 Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati wa watu akapanda juu ya mkuyu ili amwone Yesu, kwa sababu angeipitia njia ile. |
| BSB 5 When Jesus came to that place, He looked up and said, “Zacchaeus, hurry down, for I must stay at your house today.” | SWKCV 5 Yesu alipofika pale chini ya huo mkuyu, akatazama juu, akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani kwako!” |
| BSB 6 So Zacchaeus hurried down and welcomed Him joyfully. | SWKCV 6 Hivyo Zakayo akashuka upesi, akamkaribisha Yesu nyumbani kwake kwa furaha kubwa. |
| BSB 7 And all who saw this began to grumble, saying, “He has gone to be the guest of a sinful man!” | SWKCV 7 Watu wote walipoona hivyo, wakaanza kunungʼunika wakisema, “Amekwenda kuwa mgeni wa ‘mtu mwenye dhambi.’” |
| BSB 8 But Zacchaeus stood up and said to the Lord, “Look, Lord, half of my possessions I give to the poor, and if I have cheated anyone, I will repay it fourfold.” | SWKCV 8 Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana, “Tazama, Bwana! Sasa hivi nusu ya mali yangu ninawapa maskini, nami kama nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, nitamrudishia mara nne ya hicho kiwango.” |
| BSB 9 Jesus said to him, “Today salvation has come to this house, because this man too is a son of Abraham. | SWKCV 9 Ndipo Yesu akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Abrahamu. |
| BSB 10 For the Son of Man came to seek and to save the lost.” | SWKCV 10 Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” |
| BSB 11 While the people were listening to this, Jesus proceeded to tell them a parable, because He was near Jerusalem and they thought the kingdom of God would appear imminently. | SWKCV 11 Walipokuwa wanasikiliza haya, Yesu akaendelea kuwaambia mfano, kwa sababu alikuwa anakaribia Yerusalemu na watu walikuwa wakidhani ya kuwa Ufalme wa Mungu ulikuwa unakuja saa iyo hiyo. |
| BSB 12 So He said, “A man of noble birth went to a distant country to lay claim to his kingship and then return. | SWKCV 12 Hivyo akawaambia: “Mtu mmoja mwenye cheo kikubwa alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi. |
| BSB 13 Beforehand, he called ten of his servants and gave them ten minas. ‘Conduct business with this until I return,’ he said. | SWKCV 13 Hivyo akawaita kumi miongoni mwa watumishi wake, na akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Fanyeni biashara na fedha hizi mpaka nitakaporudi.’ |
| BSB 14 But his subjects hated him and sent a delegation after him to say, ‘We do not want this man to rule over us.’ | SWKCV 14 “Lakini raiya wa nchi yake walimchukia wakapeleka ujumbe na kusema, ‘Hatutaki huyu mtu awe mfalme wetu.’ |
| BSB 15 When he returned from procuring his kingship, he summoned the servants to whom he had given the money, to find out what each one had earned. | SWKCV 15 “Hata hivyo alirudi akiwa amekwisha kupokea mamlaka ya ufalme, akawaita wale watumishi wake aliokuwa amewaachia fedha, ili afahamu ni faida kiasi gani kila mmoja wao aliyopata kwa kufanya biashara. |
| BSB 16 The first servant came forward and said, ‘Master, your mina has produced ten more minas.’ | SWKCV 16 “Wa kwanza akaja na kusema, ‘Bwana, kutokana na fedha uliyoniachia, nimepata faida mara kumi zaidi.’ |
| BSB 17 His master replied, ‘Well done, good servant! Because you have been faithful in a very small matter, you shall have authority over ten cities.’ | SWKCV 17 “Yule bwana akamjibu, ‘Umefanya vizuri mtumishi mwema! Kwa sababu umekuwa mwaminifu katika wajibu mdogo sana, nakupa mamlaka juu ya miji kumi.’ |
| BSB 18 The second servant came and said, ‘Master, your mina has made five minas.’ | SWKCV 18 “Wa pili naye akaja. Akasema, ‘Bwana, fedha yako imeleta faida mara tano zaidi.’ |
| BSB 19 And to this one he said, ‘You shall have authority over five cities.’ | SWKCV 19 “Bwana wake akajibu, ‘Nakupa mamlaka juu ya miji mitano.’ |
| BSB 20 Then another servant came and said, ‘Master, here is your mina, which I have laid away in a piece of cloth. | SWKCV 20 “Kisha akaja yule mtumishi mwingine, akasema, ‘Bwana, hii hapa fedha yako. Niliitunza vizuri kwenye kitambaa. |
| BSB 21 For I was afraid of you, because you are a harsh man. You withdraw what you did not deposit and reap what you did not sow.’ | SWKCV 21 Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mgumu. Unachukua ambapo hukuweka kitu, na unavuna mahali ambapo hukupanda kitu.’ |
| BSB 22 His master replied, ‘You wicked servant, I will judge you by your own words. So you knew that I am a harsh man, withdrawing what I did not deposit and reaping what I did not sow? | SWKCV 22 “Bwana wake akamjibu, ‘Nitakuhukumu kwa maneno yako mwenyewe, wewe mtumishi mwovu! Kama ulifahamu kwamba mimi ni mtu mgumu, nichukuaye mahali ambapo sikuweka kitu na kuvuna mahali ambapo sikupanda, |
| BSB 23 Why then did you not deposit my money in the bank, and upon my return I could have collected it with interest?’ | SWKCV 23 kwa nini basi hukuweka fedha zangu kwa watoa riba, ili nitakaporudi nichukue iliyo yangu na riba yake?’ |
| BSB 24 Then he told those standing by, ‘Take the mina from him and give it to the one who has ten minas.’ | SWKCV 24 “Ndipo akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu, ‘Mnyangʼanyeni fungu lake la fedha, mkampe yule mwenye kumi.’ |
| BSB 25 ‘Master,’ they said, ‘he already has ten!’ | SWKCV 25 “Wakamwambia, ‘Bwana, mbona; tayari anayo mafungu kumi!’ |
| BSB 26 He replied, ‘I tell you that everyone who has will be given more; but the one who does not have, even what he has will be taken away from him. | SWKCV 26 “Akawajibu, ‘Nawaambia kwamba kila aliye na kitu, ataongezewa. Lakini yule asiye na kitu, hata alicho nacho atanyangʼanywa. |
| BSB 27 And these enemies of mine who were unwilling for me to rule over them, bring them here and slay them in front of me.’” | SWKCV 27 Lakini wale adui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme juu yao. Waleteni hapa mkawaue mbele yangu.’” |
| BSB 28 After Jesus had said this, He went on ahead, going up to Jerusalem. | SWKCV 28 Baada ya Yesu kusema haya, alitangulia kupanda kwenda Yerusalemu. |
| BSB 29 As He approached Bethphage and Bethany at the Mount of Olives, He sent out two of His disciples, | SWKCV 29 Naye alipokaribia Bethfage na Bethania kwenye mlima uitwao Mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili, akawaambia, |
| BSB 30 saying, “Go into the village ahead of you, and as you enter it, you will find a colt tied there, on which no one has ever sat. Untie it and bring it here. | SWKCV 30 “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu. Na mtakapokuwa mnaingia kijijini, mtamkuta mwana-punda amefungwa hapo, ambaye hajapandwa na mtu bado. Mfungueni, mkamlete hapa. |
| BSB 31 If anyone asks, ‘Why are you untying it?’ tell him, ‘The Lord needs it.’” | SWKCV 31 Kama mtu akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Mwambieni, ‘Bwana anamhitaji.’” |
| BSB 32 So those who were sent went out and found it just as Jesus had told them. | SWKCV 32 Wale waliotumwa wakaenda, wakakuta kila kitu kama vile Yesu alivyokuwa amewaambia. |
| BSB 33 As they were untying the colt, its owners asked, “Why are you untying the colt?” | SWKCV 33 Walipokuwa wanamfungua yule mwana-punda, wenyewe wakawauliza, “Mbona mnamfungua huyo mwana-punda?” |
| BSB 34 “The Lord needs it,” they answered. | SWKCV 34 Wale wanafunzi wakajibu, “Bwana anamhitaji.” |
| BSB 35 Then they led the colt to Jesus, threw their cloaks over it, and put Jesus on it. | SWKCV 35 Wakamleta kwa Yesu, nao baada ya kutandika mavazi yao juu ya huyo mwana-punda, wakampandisha Yesu juu yake. |
| BSB 36 As He rode along, the people spread their cloaks on the road. | SWKCV 36 Alipokuwa akienda akiwa amempanda, watu wakatandaza mavazi yao barabarani. |
| BSB 37 And as He approached the descent from the Mount of Olives, the whole multitude of disciples began to praise God joyfully in a loud voice for all the miracles they had seen: | SWKCV 37 Alipokaribia mahali yanapoanzia materemko ya Mlima wa Mizeituni, umati wote wa wafuasi wake wakaanza kumsifu Mungu kwa furaha kwa sauti kuu kwa ajili ya matendo yote ya miujiza waliyoyaona. Wakasema: |
| BSB 38 “Blessed is the King who comes in the name of the Lord!” “Peace in heaven and glory in the highest!” | SWKCV 38 “Amebarikiwa Mfalme ajaye kwa Jina la Bwana!” “Amani mbinguni na utukufu huko juu sana.” |
| BSB 39 But some of the Pharisees in the crowd said to Him, “Teacher, rebuke Your disciples!” | SWKCV 39 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwamo miongoni mwa ule umati wa watu wakamwambia, “Mwalimu, waamuru wanafunzi wako wanyamaze.” |
| BSB 40 “I tell you,” He answered, “if they remain silent, the very stones will cry out.” | SWKCV 40 Yesu akawajibu, “Nawaambia ninyi, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele.” |
| BSB 41 As Jesus approached Jerusalem and saw the city, He wept over it | SWKCV 41 Alipokaribia Yerusalemu na kuuona mji, aliulilia, |
| BSB 42 and said, “If only you had known on this day what would bring you peace! But now it is hidden from your eyes. | SWKCV 42 akisema, “Laiti ungalijua hata wewe leo yale ambayo yangeleta amani, lakini sasa yamefichika machoni pako. |
| BSB 43 For the days will come upon you when your enemies will barricade you and surround you and hem you in on every side. | SWKCV 43 Hakika siku zinakujia, ambazo adui zako watakuzingira, nao watakuzunguka pande zote na kukuzuilia ndani. |
| BSB 44 They will level you to the ground—you and the children within your walls. They will not leave one stone on another, because you did not recognize the time of your visitation from God.” | SWKCV 44 Watakuponda chini, wewe na watoto walioko ndani ya kuta zako. Nao hawataacha hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu hukutambua wakati wa kujiliwa kwako.” |
| BSB 45 Then Jesus entered the temple courts and began to drive out those who were selling there. | SWKCV 45 Ndipo akaingia eneo la Hekalu, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza vitu humo. |
| BSB 46 He declared to them, “It is written: ‘My house will be a house of prayer.’ But you have made it ‘a den of robbers.’” | SWKCV 46 Naye akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa ‘pango la wanyangʼanyi.’” |
| BSB 47 Jesus was teaching at the temple every day, but the chief priests, scribes, and leaders of the people were intent on killing Him. | SWKCV 47 Kila siku alikuwa akifundisha Hekaluni. Lakini viongozi wa makuhani, walimu wa sheria na viongozi wa watu walikuwa wakitafuta njia ili kumuua. |
| BSB 48 Yet they could not find a way to do so, because all the people hung on His words. | SWKCV 48 Lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote walimfuata wakiyasikiliza maneno yake kwa usikivu mwingi. |
Questions about Luke 19? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.