Luke 20
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 One day as Jesus was teaching the people in the temple courts and proclaiming the gospel, the chief priests and scribes, together with the elders, came up to Him. | SWKCV 1 Siku moja, Yesu alipokuwa akifundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, pamoja na wazee wa watu wakamjia. |
| BSB 2 “Tell us,” they said, “by what authority are You doing these things, and who gave You this authority?” | SWKCV 2 Wakamuuliza, “Tuambie, unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Ni nani aliyekupa mamlaka haya?” |
| BSB 3 “I will also ask you a question,” Jesus replied. “Tell Me: | SWKCV 3 Akawajibu, “Nami nitawauliza swali. |
| BSB 4 John’s baptism—was it from heaven, or from men?” | SWKCV 4 Je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?” |
| BSB 5 They deliberated among themselves and said, “If we say, ‘From heaven,’ He will ask, ‘Why did you not believe him?’ | SWKCV 5 Wakahojiana wao kwa wao wakisema, “Kama tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ |
| BSB 6 But if we say, ‘From men,’ all the people will stone us, for they are convinced that John was a prophet.” | SWKCV 6 Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ watu wote watatupiga mawe, kwa sababu wanaamini kwamba Yohana alikuwa nabii.” |
| BSB 7 So they answered that they did not know where it was from. | SWKCV 7 Basi wakajibu, “Hatujui ulikotoka.” |
| BSB 8 And Jesus replied, “Neither will I tell you by what authority I am doing these things.” | SWKCV 8 Yesu akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.” |
| BSB 9 Then He proceeded to tell the people this parable: “A man planted a vineyard, rented it out to some tenants, and went away for a long time. | SWKCV 9 Akaendelea kuwaambia watu mfano huu: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwa muda mrefu. |
| BSB 10 At harvest time, he sent a servant to the tenants to collect his share of the fruit of the vineyard. But the tenants beat the servant and sent him away empty-handed. | SWKCV 10 Wakati wa mavuno ulipofika, akamtuma mtumishi wake kwa hao wapangaji ili wampe sehemu ya mavuno ya shamba la mizabibu. Lakini wale wakulima wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. |
| BSB 11 So he sent another servant, but they beat him and treated him shamefully, sending him away empty-handed. | SWKCV 11 Akamtuma mtumishi mwingine, huyo naye wakampiga, wakamfanyia mambo ya aibu na kumfukuza. |
| BSB 12 Then he sent a third, but they wounded him and threw him out. | SWKCV 12 Bado akamtuma na mwingine wa tatu, huyu pia wakamjeruhi na kumtupa nje ya shamba. |
| BSB 13 ‘What shall I do?’ asked the owner of the vineyard. ‘I will send my beloved son. Perhaps they will respect him.’ | SWKCV 13 “Basi yule mwenye shamba la mizabibu akasema, ‘Nifanye nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa, huenda yeye watamheshimu.’ |
| BSB 14 But when the tenants saw the son, they discussed it among themselves and said, ‘This is the heir. Let us kill him, and the inheritance will be ours.’ | SWKCV 14 “Lakini wale wapangaji walipomwona, wakasemezana wao kwa wao. Wakasema, ‘Huyu ndiye mrithi. Basi na tumuue ili urithi uwe wetu.’ |
| BSB 15 So they threw him out of the vineyard and killed him. What then will the owner of the vineyard do to them? | SWKCV 15 Kwa hiyo wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua.” “Sasa basi yule mwenye shamba la mizabibu atawafanyia nini wapangaji hawa? |
| BSB 16 He will come and kill those tenants and give the vineyard to others.” And when the people heard this, they said, “May such a thing never happen!” | SWKCV 16 Atakuja na kuwaua hao wapangaji, na kuwapa wapangaji wengine hilo shamba la mizabibu.” Watu waliposikia hayo wakasema, “Mungu apishie mbali jambo hili lisitokee!” |
| BSB 17 But Jesus looked directly at them and said, “Then what is the meaning of that which is written: ‘The stone the builders rejected has become the cornerstone’? | SWKCV 17 Lakini Yesu akawakazia macho, akasema, “Basi ni nini maana ya yale yaliyoandikwa: “ ‘Jiwe walilolikataa waashi, limekuwa jiwe kuu la pembeni’? |
| BSB 18 Everyone who falls on this stone will be broken to pieces, but he on whom it falls will be crushed.” | SWKCV 18 Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.” |
| BSB 19 When the scribes and chief priests realized that Jesus had spoken this parable against them, they sought to arrest Him that very hour. But they were afraid of the people. | SWKCV 19 Walimu wa sheria na viongozi wa makuhani wakatafuta njia ya kumkamata mara moja, kwa sababu walifahamu kwamba amesema mfano huo kwa ajili yao. Lakini waliwaogopa watu. |
| BSB 20 So they watched Him closely and sent spies who pretended to be sincere. They were hoping to catch Him in His words in order to hand Him over to the rule and authority of the governor. | SWKCV 20 Kwa hiyo wakawa wanamchunguza na kutuma wapelelezi waliojifanya kuwa wenye haki ili wapate kumtega kwa maneno asemayo, ili wamtie katika uwezo na mamlaka ya mtawala. |
| BSB 21 “Teacher,” they inquired, “we know that You speak and teach correctly. You show no partiality but teach the way of God in accordance with the truth. | SWKCV 21 Hivyo wale wapelelezi wakamuuliza, “Mwalimu, tunajua unasema na kufundisha yaliyo kweli wala humpendelei mtu, bali wafundisha njia ya Mungu katika kweli. |
| BSB 22 Is it lawful for us to pay taxes to Caesar or not?” | SWKCV 22 Je, ni halali sisi kulipa kodi kwa Kaisari, au la?” |
| BSB 23 But Jesus saw through their duplicity and said to them, | SWKCV 23 Lakini Yesu akatambua hila yao, kwa hiyo akawaambia, |
| BSB 24 “Show Me a denarius. Whose image and inscription are on it?” “Caesar’s,” they answered. | SWKCV 24 “Nionyesheni dinari. Je, sura hii na maandishi haya yaliyoko juu yake ni vya nani?” |
| BSB 25 So Jesus told them, “Give to Caesar what is Caesar’s, and to God what is God’s.” | SWKCV 25 Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Akawaambia, “Basi mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.” |
| BSB 26 And they were unable to trap Him in His words before the people. And amazed at His answer, they fell silent. | SWKCV 26 Wakashindwa kumkamata kwa yale aliyokuwa amesema hadharani. Nao wakashangazwa mno na majibu yake, wakanyamaza kimya. |
| BSB 27 Then some of the Sadducees, who say there is no resurrection, came to question Him. | SWKCV 27 Baadhi ya Masadukayo, wale wasemao kwamba hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Yesu na kumuuliza, |
| BSB 28 “Teacher,” they said, “Moses wrote for us that if a man’s brother dies and leaves a wife but no children, the man is to marry his brother’s widow and raise up offspring for him. | SWKCV 28 “Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto. |
| BSB 29 Now there were seven brothers. The first one married a wife but died childless. | SWKCV 29 Basi palikuwepo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa, akafa bila kuzaa mtoto. |
| BSB 30 Then the second | SWKCV 30 Kisha yule wa pili akamwoa huyo mjane, naye akafa bila mtoto, |
| BSB 31 and the third married the widow, and in the same way all seven died, leaving no children. | SWKCV 31 naye wa tatu pia akamwoa. Vivyo hivyo ndugu wote saba wakawa wamemwoa huyo mwanamke, na wote wakafa pasipo yeyote kupata mtoto. |
| BSB 32 And last of all, the woman died. | SWKCV 32 Mwishowe, yule mwanamke naye akafa. |
| BSB 33 So then, in the resurrection, whose wife will she be? For all seven were married to her.” | SWKCV 33 Sasa basi, siku ya ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani, maana aliolewa na ndugu wote saba?” |
| BSB 34 Jesus answered, “The sons of this age marry and are given in marriage. | SWKCV 34 Yesu akawajibu, “Katika maisha haya watu huoa na kuolewa. |
| BSB 35 But those who are considered worthy to share in the age to come and in the resurrection from the dead will neither marry nor be given in marriage. | SWKCV 35 Lakini wale ambao wamehesabiwa kwamba wanastahili kupata nafasi katika ulimwengu ule na katika ufufuo wa wafu, hawaoi wala hawaolewi. |
| BSB 36 In fact, they can no longer die, because they are like the angels. And since they are sons of the resurrection, they are sons of God. | SWKCV 36 Hawa hawawezi kufa tena, kwa maana wao ni kama malaika. Wao ni watoto wa Mungu, kwa sababu ni watoto wa ufufuo. |
| BSB 37 Even Moses demonstrates that the dead are raised, in the passage about the burning bush. For he calls the Lord ‘the God of Abraham, the God of Isaac, and the God of Jacob.’ | SWKCV 37 Hata Mose alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Bwana, ‘Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo.’ |
| BSB 38 He is not the God of the dead, but of the living, for to Him all are alive.” | SWKCV 38 Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa kuwa kwake wote ni hai.” |
| BSB 39 Some of the scribes answered, “Teacher, You have spoken well!” | SWKCV 39 Baadhi ya walimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umesema sawasawa kabisa!” |
| BSB 40 And they did not dare to question Him any further. | SWKCV 40 Baada ya hayo hakuna mtu aliyethubutu kumuuliza maswali tena. |
| BSB 41 Then Jesus declared, “How can it be said that the Christ is the Son of David? | SWKCV 41 Kisha Yesu akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Kristo ni Mwana wa Daudi? |
| BSB 42 For David himself says in the book of Psalms: ‘The Lord said to my Lord, “Sit at My right hand | SWKCV 42 Daudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, |
| BSB 43 until I make Your enemies a footstool for Your feet.”’ | SWKCV 43 hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.”’ |
| BSB 44 Thus David calls Him ‘Lord.’ So how can He be David’s son?” | SWKCV 44 Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?” |
| BSB 45 In the hearing of all the people, Jesus said to His disciples, | SWKCV 45 Wakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Yesu akawaambia wanafunzi wake, |
| BSB 46 “Beware of the scribes. They like to walk around in long robes, and they love the greetings in the marketplaces, the chief seats in the synagogues, and the places of honor at banquets. | SWKCV 46 “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu. |
| BSB 47 They defraud widows of their houses, and for a show make lengthy prayers. These men will receive greater condemnation.” | SWKCV 47 Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.” |
Questions about Luke 20? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.