Psalms 139
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 For the choirmaster. A Psalm of David. O LORD, You have searched me and known me. | SWKCV 1 Ee Bwana, umenichunguza na kunijua. |
| BSB 2 You know when I sit and when I rise; You understand my thoughts from afar. | SWKCV 2 Unajua ninapoketi na ninapoinuka; unatambua mawazo yangu tokea mbali. |
| BSB 3 You search out my path and my lying down; You are aware of all my ways. | SWKCV 3 Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote. |
| BSB 4 Even before a word is on my tongue, You know all about it, O LORD. | SWKCV 4 Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana. |
| BSB 5 You hem me in behind and before; You have laid Your hand upon me. | SWKCV 5 Umenizunguka nyuma na mbele; umeweka mkono wako juu yangu. |
| BSB 6 Such knowledge is too wonderful for me, too lofty for me to attain. | SWKCV 6 Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu, ni ya juu sana kwangu kuyafikia. |
| BSB 7 Where can I go to escape Your Spirit? Where can I flee from Your presence? | SWKCV 7 Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? |
| BSB 8 If I ascend to the heavens, You are there; if I make my bed in Sheol, You are there. | SWKCV 8 Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko. |
| BSB 9 If I rise on the wings of the dawn, if I settle by the farthest sea, | SWKCV 9 Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko, kama nikikaa pande za mbali za bahari, |
| BSB 10 even there Your hand will guide me; Your right hand will hold me fast. | SWKCV 10 hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti. |
| BSB 11 If I say, “Surely the darkness will hide me, and the light become night around me”— | SWKCV 11 Kama nikisema, “Hakika giza litanificha na nuru inayonizunguka iwe usiku,” |
| BSB 12 even the darkness is not dark to You, but the night shines like the day, for darkness is as light to You. | SWKCV 12 hata giza halitakuwa giza kwako, usiku utangʼaa kama mchana, kwa kuwa giza ni kama nuru kwako. |
| BSB 13 For You formed my inmost being; You knit me together in my mother’s womb. | SWKCV 13 Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani; uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu. |
| BSB 14 I praise You, for I am fearfully and wonderfully made. Marvelous are Your works, and I know this very well. | SWKCV 14 Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa kwa namna ya ajabu na ya kutisha; kazi zako ni za ajabu, ninajua hayo kikamilifu. |
| BSB 15 My frame was not hidden from You when I was made in secret, when I was woven together in the depths of the earth. | SWKCV 15 Umbile langu halikufichika kwako, nilipoumbwa mahali pa siri. Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi, |
| BSB 16 Your eyes saw my unformed body; all my days were written in Your book and ordained for me before one of them came to be. | SWKCV 16 macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. Siku zangu zote ulizonipangia ziliandikwa katika kitabu chako kabla haijakuwepo hata moja. |
| BSB 17 How precious to me are Your thoughts, O God, how vast is their sum! | SWKCV 17 Tazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu! Jinsi jumla yake ilivyo kubwa! |
| BSB 18 If I were to count them, they would outnumber the grains of sand; and when I awake, I am still with You. | SWKCV 18 Kama ningezihesabu, zingekuwa nyingi kuliko mchanga. Niamkapo, bado niko pamoja nawe. |
| BSB 19 O God, that You would slay the wicked—away from me, you bloodthirsty men— | SWKCV 19 Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu! |
| BSB 20 who speak of You deceitfully; Your enemies take Your name in vain. | SWKCV 20 Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya, adui zako wanatumia vibaya jina lako. |
| BSB 21 Do I not hate those who hate You, O LORD, and detest those who rise against You? | SWKCV 21 Ee Bwana, je, nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako? |
| BSB 22 I hate them with perfect hatred; I count them as my enemies. | SWKCV 22 Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao, ninawahesabu ni adui zangu. |
| BSB 23 Search me, O God, and know my heart; test me and know my concerns. | SWKCV 23 Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, nijaribu na ujue mawazo yangu. |
| BSB 24 See if there is any offensive way in me; lead me in the way everlasting. | SWKCV 24 Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele. |
Questions about Psalms 139? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.