Psalms 22
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 For the choirmaster. To the tune of “The Doe of the Dawn.” A Psalm of David. My God, my God, why have You forsaken me? Why are You so far from saving me, so far from my words of groaning? | SWKCV 1 Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa? Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu? |
| BSB 2 I cry out by day, O my God, but You do not answer, and by night, but I have no rest. | SWKCV 2 Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, hata usiku, sinyamazi. |
| BSB 3 Yet You are holy, enthroned on the praises of Israel. | SWKCV 3 Hata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Uliye Mtakatifu; wewe ni sifa ya Israeli. |
| BSB 4 In You our fathers trusted; they trusted and You delivered them. | SWKCV 4 Kwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao, walikutumaini nawe ukawaokoa. |
| BSB 5 They cried out to You and were set free; they trusted in You and were not disappointed. | SWKCV 5 Walikulilia wewe na ukawaokoa, walikutegemea wewe nao hawakuaibika. |
| BSB 6 But I am a worm and not a man, scorned by men and despised by the people. | SWKCV 6 Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau. |
| BSB 7 All who see me mock me; they sneer and shake their heads: | SWKCV 7 Wote wanionao hunidhihaki, hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao: |
| BSB 8 “He trusts in the LORD, let the LORD deliver him; let the LORD rescue him, since He delights in him.” | SWKCV 8 Husema, “Anamtegemea Bwana, basi Bwana na amwokoe. Amkomboe basi, kwa maana anapendezwa naye.” |
| BSB 9 Yet You brought me forth from the womb; You made me secure at my mother’s breast. | SWKCV 9 Hata hivyo ulinitoa tumboni, ukanifanya nikutegemee, hata nilipokuwa ninanyonya matiti ya mama yangu. |
| BSB 10 From birth I was cast upon You; from my mother’s womb You have been my God. | SWKCV 10 Nimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa, toka tumboni mwa mama yangu umekuwa Mungu wangu. |
| BSB 11 Be not far from me, for trouble is near and there is no one to help. | SWKCV 11 Usiwe mbali nami, kwa maana shida iko karibu na hakuna wa kunisaidia. |
| BSB 12 Many bulls surround me; strong bulls of Bashan encircle me. | SWKCV 12 Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira. |
| BSB 13 They open their jaws against me like lions that roar and maul. | SWKCV 13 Simba wangurumao wanaorarua mawindo yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu. |
| BSB 14 I am poured out like water, and all my bones are disjointed. My heart is like wax; it melts away within me. | SWKCV 14 Nimemiminwa kama maji, mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake. Moyo wangu umegeuka kuwa nta, umeyeyuka ndani yangu. |
| BSB 15 My strength is dried up like a potsherd, and my tongue sticks to the roof of my mouth. You lay me in the dust of death. | SWKCV 15 Nguvu zangu zimekauka kama kigae, ulimi wangu umegandamana na kaakaa la kinywa changu, kwa sababu umenilaza katika mavumbi ya kifo. |
| BSB 16 For dogs surround me; a band of evil men encircles me; they have pierced my hands and feet. | SWKCV 16 Mbwa wamenizunguka, kundi la watu waovu limenizingira, wametoboa mikono yangu na miguu yangu. |
| BSB 17 I can count all my bones; they stare and gloat over me. | SWKCV 17 Naweza kuhesabu mifupa yangu yote, watu wananikodolea macho na kunisimanga. |
| BSB 18 They divide my garments among them and cast lots for my clothing. | SWKCV 18 Wanagawana nguo zangu wao kwa wao, na vazi langu wanalipigia kura. |
| BSB 19 But You, O LORD, be not far off; O my Strength, come quickly to help me. | SWKCV 19 Lakini wewe, Ee Bwana, usiwe mbali. Ee Nguvu yangu, uje haraka unisaidie. |
| BSB 20 Deliver my soul from the sword, my precious life from the power of wild dogs. | SWKCV 20 Okoa maisha yangu na upanga, uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa. |
| BSB 21 Save me from the mouth of the lion; at the horns of the wild oxen You have answered me! | SWKCV 21 Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu. |
| BSB 22 I will proclaim Your name to my brothers; I will praise You in the assembly. | SWKCV 22 Nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu, katika kusanyiko nitakusifu wewe. |
| BSB 23 You who fear the LORD, praise Him! All descendants of Jacob, honor Him! All offspring of Israel, revere Him! | SWKCV 23 Ninyi ambao mnamcha Bwana, msifuni! Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye! Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli! |
| BSB 24 For He has not despised or detested the torment of the afflicted. He has not hidden His face from him, but has attended to his cry for help. | SWKCV 24 Kwa maana hakupuuza wala kudharau mateso ya aliyeonewa; hakumficha uso wake bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie. |
| BSB 25 My praise for You resounds in the great assembly; I will fulfill my vows before those who fear You. | SWKCV 25 Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa, nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe. |
| BSB 26 The poor will eat and be satisfied; those who seek the LORD will praise Him. May your hearts live forever! | SWKCV 26 Maskini watakula na kushiba, wale wamtafutao Bwana watamsifu: mioyo yenu na iishi milele! |
| BSB 27 All the ends of the earth will remember and turn to the LORD. All the families of the nations will bow down before Him. | SWKCV 27 Miisho yote ya dunia itakumbuka na kumgeukia Bwana, nazo jamaa zote za mataifa watasujudu mbele zake, |
| BSB 28 For dominion belongs to the LORD and He rules over the nations. | SWKCV 28 kwa maana ufalme ni wa Bwana naye hutawala juu ya mataifa. |
| BSB 29 All the rich of the earth will feast and worship; all who go down to the dust will kneel before Him—even those unable to preserve their lives. | SWKCV 29 Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu. Wote waendao mavumbini watapiga magoti mbele yake, wote ambao hawawezi kudumisha uhai wao. |
| BSB 30 Posterity will serve Him; they will declare the Lord to a new generation. | SWKCV 30 Wazao wa baadaye watamtumikia yeye; vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana. |
| BSB 31 They will come and proclaim His righteousness to a people yet unborn—all that He has done. | SWKCV 31 Watatangaza haki yake kwa watu ambao hawajazaliwa bado, kwa maana yeye ametenda hili. |
Questions about Psalms 22? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.