Psalms 41
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 For the choirmaster. A Psalm of David. Blessed is the one who cares for the poor; the LORD will deliver him in the day of trouble. | SWKCV 1 Heri mtu yule anayemjali mnyonge, Bwana atamwokoa wakati wa shida. |
| BSB 2 The LORD will protect and preserve him; He will bless him in the land and refuse to give him over to the will of his foes. | SWKCV 2 Bwana atamlinda na kuyahifadhi maisha yake, atambariki katika nchi na hatamwacha katika tamaa ya adui zake. |
| BSB 3 The LORD will sustain him on his bed of illness and restore him from his bed of sickness. | SWKCV 3 Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani, atamwinua kutoka kitandani mwake. |
| BSB 4 I said, “O LORD, be gracious to me; heal me, for I have sinned against You.” | SWKCV 4 Nilisema, “Ee Bwana nihurumie, niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.” |
| BSB 5 My enemies say with malice: “When will he die and be forgotten?” | SWKCV 5 Adui zangu wanasema kwa hila, “Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.” |
| BSB 6 My visitor speaks falsehood; he gathers slander in his heart; he goes out and spreads it abroad. | SWKCV 6 Kila anapokuja mtu kunitazama, huzungumza uongo, huku moyo wake hukusanya masingizio; kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko. |
| BSB 7 All who hate me whisper against me; they imagine the worst for me: | SWKCV 7 Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu, hao huniwazia mabaya sana, wakisema, |
| BSB 8 “A vile disease has been poured into him; he will never get up from where he lies!” | SWKCV 8 “Ugonjwa mbaya sana umempata, kamwe hatainuka tena kitandani mwake.” |
| BSB 9 Even my close friend whom I trusted, the one who shared my bread, has lifted up his heel against me. | SWKCV 9 Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini, yule aliyekula chakula changu ameniinulia kisigino chake. |
| BSB 10 But You, O LORD, be gracious to me and raise me up, that I may repay them. | SWKCV 10 Lakini wewe, Ee Bwana, nihurumie, ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi. |
| BSB 11 By this I know that You delight in me, for my enemy does not triumph over me. | SWKCV 11 Najua kwamba wapendezwa nami, kwa kuwa adui yangu hanishindi. |
| BSB 12 In my integrity You uphold me and set me in Your presence forever. | SWKCV 12 Katika uadilifu wangu unanitegemeza na kuniweka kwenye uwepo wako milele. |
| BSB 13 Blessed be the LORD, the God of Israel, from everlasting to everlasting. Amen and Amen. | SWKCV 13 Msifuni Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Amen na Amen. |
Questions about Psalms 41? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.