Psalms 78
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 A Maskil of Asaph. Give ear, O my people, to my instruction; listen to the words of my mouth. | SWKCV 1 Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu, sikilizeni maneno ya kinywa changu. |
| BSB 2 I will open my mouth in parables; I will utter things hidden from the beginning, | SWKCV 2 Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo, nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale: |
| BSB 3 that we have heard and known and our fathers have relayed to us. | SWKCV 3 yale ambayo tuliyasikia na kuyajua, yale ambayo baba zetu walituambia. |
| BSB 4 We will not hide them from their children but will declare to the next generation the praises of the LORD and His might and the wonders He has performed. | SWKCV 4 Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya. |
| BSB 5 For He established a testimony in Jacob and appointed a law in Israel, which He commanded our fathers to teach to their children, | SWKCV 5 Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao, |
| BSB 6 that the coming generation would know them—even children yet to be born—to arise and tell their own children | SWKCV 6 ili kizazi kijacho kizijue, pamoja na watoto ambao watazaliwa, nao pia wapate kuwaeleza watoto wao. |
| BSB 7 that they should put their confidence in God, not forgetting His works, but keeping His commandments. | SWKCV 7 Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu, nao wasingesahau matendo yake, bali wangalizishika amri zake. |
| BSB 8 Then they will not be like their fathers, a stubborn and rebellious generation, whose heart was not loyal, whose spirit was not faithful to God. | SWKCV 8 Ili wasifanane na baba zao, waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi, ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwake, ambao roho zao hazikumwamini. |
| BSB 9 The archers of Ephraim turned back on the day of battle. | SWKCV 9 Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, walikimbia siku ya vita. |
| BSB 10 They failed to keep God’s covenant and refused to live by His law. | SWKCV 10 Hawakulishika agano la Mungu na walikataa kuishi kwa sheria yake. |
| BSB 11 They forgot what He had done, the wonders He had shown them. | SWKCV 11 Walisahau aliyokuwa ameyatenda, maajabu aliyokuwa amewaonyesha. |
| BSB 12 He worked wonders before their fathers in the land of Egypt, in the region of Zoan. | SWKCV 12 Alitenda miujiza machoni mwa baba zao, huko Soani, katika nchi ya Misri. |
| BSB 13 He split the sea and brought them through; He set the waters upright like a wall. | SWKCV 13 Aliigawanya bahari akawapitisha, alifanya maji yasimame imara kama ukuta. |
| BSB 14 He led them with a cloud by day and with a light of fire all night. | SWKCV 14 Aliwaongoza kwa wingu mchana na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha. |
| BSB 15 He split the rocks in the wilderness and gave them drink as abundant as the seas. | SWKCV 15 Alipasua miamba jangwani na akawapa maji tele kama bahari, |
| BSB 16 He brought streams from the stone and made water flow down like rivers. | SWKCV 16 alitoa vijito kutoka kwenye jabali lililochongoka, akayafanya maji yatiririke kama mito. |
| BSB 17 But they continued to sin against Him, rebelling in the desert against the Most High. | SWKCV 17 Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana. |
| BSB 18 They willfully tested God by demanding the food they craved. | SWKCV 18 Kwa makusudi walimjaribu Mungu, wakidai vyakula walivyovitamani. |
| BSB 19 They spoke against God, saying, “Can God really prepare a table in the wilderness? | SWKCV 19 Walinena dhidi ya Mungu, wakisema, “Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani? |
| BSB 20 When He struck the rock, water gushed out and torrents raged. But can He also give bread or supply His people with meat?” | SWKCV 20 Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu, vijito vikatiririka maji mengi. Lakini je, aweza kutupa chakula pia? Je, anaweza kuwapa watu wake nyama?” |
| BSB 21 Therefore the LORD heard and was filled with wrath; so a fire was kindled against Jacob, and His anger flared against Israel, | SWKCV 21 Bwana alipowasikia, alikasirika sana, moto wake ukawa dhidi ya Yakobo, na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli, |
| BSB 22 because they did not believe God or rely on His salvation. | SWKCV 22 kwa kuwa hawakumwamini Mungu, wala kuutumainia ukombozi wake. |
| BSB 23 Yet He commanded the clouds above and opened the doors of the heavens. | SWKCV 23 Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu na kufungua milango ya mbingu, |
| BSB 24 He rained down manna for them to eat; He gave them grain from heaven. | SWKCV 24 akawanyeshea mana ili watu wale; aliwapa nafaka ya mbinguni. |
| BSB 25 Man ate the bread of angels; He sent them food in abundance. | SWKCV 25 Watu walikula mkate wa malaika, akawatumia chakula chote ambacho wangeliweza kula. |
| BSB 26 He stirred the east wind from the heavens and drove the south wind by His might. | SWKCV 26 Aliachia upepo wa mashariki kutoka kwenye mbingu na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake. |
| BSB 27 He rained meat on them like dust, and winged birds like the sand of the sea. | SWKCV 27 Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, ndege warukao kama mchanga wa pwani. |
| BSB 28 He felled them in the midst of their camp, all around their dwellings. | SWKCV 28 Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao, kuzunguka mahema yao yote. |
| BSB 29 So they ate and were well filled, for He gave them what they craved. | SWKCV 29 Walikula na kusaza, kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani. |
| BSB 30 Yet before they had filled their desire, with the food still in their mouths, | SWKCV 30 Kabla hawajamaliza kula walichokitamani, hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao, |
| BSB 31 God’s anger flared against them, and He put to death their strongest and subdued the young men of Israel. | SWKCV 31 hasira ya Mungu ikawaka juu yao, akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao, akiwaangusha vijana wa Israeli. |
| BSB 32 In spite of all this, they kept on sinning; despite His wonderful works, they did not believe. | SWKCV 32 Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi, licha ya maajabu yake, hawakuamini. |
| BSB 33 So He ended their days in futility, and their years in sudden terror. | SWKCV 33 Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili na miaka yao katika vitisho. |
| BSB 34 When He slew them, they would seek Him; they repented and searched for God. | SWKCV 34 Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao, waliosalia walimtafuta, walimgeukia tena kwa shauku. |
| BSB 35 And they remembered that God was their Rock, that God Most High was their Redeemer. | SWKCV 35 Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao, kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao. |
| BSB 36 But they deceived Him with their mouths, and lied to Him with their tongues. | SWKCV 36 Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao, |
| BSB 37 Their hearts were disloyal to Him, and they were unfaithful to His covenant. | SWKCV 37 mioyo yao haikuwa thabiti kwake, wala hawakuwa waaminifu katika agano lake. |
| BSB 38 And yet He was compassionate; He forgave their iniquity and did not destroy them. He often restrained His anger and did not unleash His full wrath. | SWKCV 38 Hata hivyo alikuwa na huruma, alisamehe maovu yao na hakuwaangamiza. Mara kwa mara alizuia hasira yake, wala hakuchochea ghadhabu yake yote. |
| BSB 39 He remembered that they were but flesh, a passing breeze that does not return. | SWKCV 39 Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi. |
| BSB 40 How often they disobeyed Him in the wilderness and grieved Him in the desert! | SWKCV 40 Mara ngapi walimwasi jangwani na kumhuzunisha nyikani! |
| BSB 41 Again and again they tested God and provoked the Holy One of Israel. | SWKCV 41 Walimjaribu Mungu mara kwa mara, wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. |
| BSB 42 They did not remember His power—the day He redeemed them from the adversary, | SWKCV 42 Hawakukumbuka uwezo wake, siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi, |
| BSB 43 when He performed His signs in Egypt and His wonders in the fields of Zoan. | SWKCV 43 siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri, maajabu yake huko Soani. |
| BSB 44 He turned their rivers to blood, and from their streams they could not drink. | SWKCV 44 Aligeuza mito yao kuwa damu, hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao. |
| BSB 45 He sent swarms of flies that devoured them, and frogs that devastated them. | SWKCV 45 Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala, na vyura wakawaharibu. |
| BSB 46 He gave their crops to the grasshopper, the fruit of their labor to the locust. | SWKCV 46 Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao, mazao yao kwa nzige. |
| BSB 47 He killed their vines with hailstones and their sycamore-figs with sleet. | SWKCV 47 Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji. |
| BSB 48 He abandoned their cattle to the hail and their livestock to bolts of lightning. | SWKCV 48 Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe, akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi. |
| BSB 49 He unleashed His fury against them, wrath, indignation, and calamity—a band of destroying angels. | SWKCV 49 Aliwafungulia hasira yake kali, ghadhabu yake, hasira na uadui, na kundi la malaika wa kuharibu. |
| BSB 50 He cleared a path for His anger; He did not spare them from death but delivered their lives to the plague. | SWKCV 50 Aliitengenezea njia hasira yake, hakuwaepusha na kifo, bali aliwaachia tauni. |
| BSB 51 He struck all the firstborn of Egypt, the virility in the tents of Ham. | SWKCV 51 Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri, matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu. |
| BSB 52 He led out His people like sheep and guided them like a flock in the wilderness. | SWKCV 52 Lakini aliwatoa watu wake kama kundi, akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani. |
| BSB 53 He led them safely, so they did not fear, but the sea engulfed their enemies. | SWKCV 53 Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa, bali bahari iliwameza adui zao. |
| BSB 54 He brought them to His holy land, to the mountain His right hand had acquired. | SWKCV 54 Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu, hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa. |
| BSB 55 He drove out nations before them and apportioned their inheritance; He settled the tribes of Israel in their tents. | SWKCV 55 Aliyafukuza mataifa mbele yao, na kuwagawia nchi zao kama urithi, aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao. |
| BSB 56 But they tested and disobeyed God Most High, for they did not keep His decrees. | SWKCV 56 Lakini wao walimjaribu Mungu, na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana, wala hawakuzishika sheria zake. |
| BSB 57 They turned back and were faithless like their fathers, twisted like a faulty bow. | SWKCV 57 Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu, wakawa wasioweza kutegemewa kama upinde wenye kasoro. |
| BSB 58 They enraged Him with their high places and provoked His jealousy with their idols. | SWKCV 58 Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu, wakachochea wivu wake kwa sanamu zao. |
| BSB 59 On hearing it, God was furious and rejected Israel completely. | SWKCV 59 Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana, akamkataa Israeli kabisa. |
| BSB 60 He abandoned the tabernacle of Shiloh, the tent He had pitched among men. | SWKCV 60 Akaiacha hema ya Shilo, hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu. |
| BSB 61 He delivered His strength to captivity, and His splendor to the hand of the adversary. | SWKCV 61 Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, utukufu wake mikononi mwa adui. |
| BSB 62 He surrendered His people to the sword because He was enraged by His heritage. | SWKCV 62 Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, akaukasirikia sana urithi wake. |
| BSB 63 Fire consumed His young men, and their maidens were left without wedding songs. | SWKCV 63 Moto uliwaangamiza vijana wao, na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi, |
| BSB 64 His priests fell by the sword, but their widows could not lament. | SWKCV 64 makuhani wao waliuawa kwa upanga, wala wajane wao hawakuweza kulia. |
| BSB 65 Then the Lord awoke as from sleep, like a mighty warrior overcome by wine. | SWKCV 65 Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini, kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo. |
| BSB 66 He beat back His foes; He put them to everlasting shame. | SWKCV 66 Aliwapiga na kuwashinda adui zake, akawatia katika aibu ya milele. |
| BSB 67 He rejected the tent of Joseph and refused the tribe of Ephraim. | SWKCV 67 Ndipo alipozikataa hema za Yosefu, hakulichagua kabila la Efraimu, |
| BSB 68 But He chose the tribe of Judah, Mount Zion, which He loved. | SWKCV 68 lakini alilichagua kabila la Yuda, Mlima Sayuni, ambao aliupenda. |
| BSB 69 He built His sanctuary like the heights, like the earth He has established forever. | SWKCV 69 Alijenga patakatifu pake kama vilele, kama dunia ambayo aliimarisha milele. |
| BSB 70 He chose David His servant and took him from the sheepfolds; | SWKCV 70 Akamchagua Daudi mtumishi wake na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo. |
| BSB 71 from tending the ewes He brought him to be shepherd of His people Jacob, of Israel His inheritance. | SWKCV 71 Kutoka kuchunga kondoo alimleta kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo, wa Israeli urithi wake. |
| BSB 72 So David shepherded them with integrity of heart and guided them with skillful hands. | SWKCV 72 Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo, kwa mikono ya ustadi aliwaongoza. |
Questions about Psalms 78? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.