Job 36
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 And Elihu continued: | SWKCV 1 Elihu akaendelea kusema: |
| BSB 2 “Bear with me a little longer, and I will show you that there is more to be said on God’s behalf. | SWKCV 2 “Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu. |
| BSB 3 I get my knowledge from afar, and I will ascribe justice to my Maker. | SWKCV 3 Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, nami nitamhesabia haki Muumba wangu. |
| BSB 4 For truly my words are free of falsehood; one perfect in knowledge is with you. | SWKCV 4 Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo; mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe. |
| BSB 5 Indeed, God is mighty, but He despises no one; He is mighty in strength of understanding. | SWKCV 5 “Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu; ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake. |
| BSB 6 He does not keep the wicked alive, but He grants justice to the afflicted. | SWKCV 6 Hawaachi waovu waendelee kuishi, bali huwapa walioteswa haki yao. |
| BSB 7 He does not take His eyes off the righteous, but He enthrones them with kings and exalts them forever. | SWKCV 7 Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki; huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme na kuwatukuza milele. |
| BSB 8 And if men are bound with chains, caught in cords of affliction, | SWKCV 8 Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo, wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso, |
| BSB 9 then He tells them their deeds and how arrogantly they have transgressed. | SWKCV 9 huwaonyesha yale waliyoyatenda, kwamba wametenda dhambi kwa majivuno. |
| BSB 10 He opens their ears to correction and commands that they turn from iniquity. | SWKCV 10 Huwafanya wao kusikia maonyo, na huwaagiza kutubu uovu wao. |
| BSB 11 If they obey and serve Him, then they end their days in prosperity and their years in happiness. | SWKCV 11 Kama wakitii na kumtumikia, wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio, na miaka yao katika utoshelevu. |
| BSB 12 But if they do not obey, then they perish by the sword and die without knowledge. | SWKCV 12 Lakini wasiposikiliza, wataangamia kwa upanga, nao watakufa pasipo maarifa. |
| BSB 13 The godless in heart harbor resentment; even when He binds them, they do not cry for help. | SWKCV 13 “Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki; hata anapowafunga, hawamwombi msaada. |
| BSB 14 They die in their youth, among the male shrine prostitutes. | SWKCV 14 Wanakufa wangali vijana, miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu. |
| BSB 15 God rescues the afflicted by their affliction and opens their ears in oppression. | SWKCV 15 Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao, na kuzungumza nao katika dhiki zao. |
| BSB 16 Indeed, He drew you from the jaws of distress to a spacious and broad place, to a table full of richness. | SWKCV 16 “Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki, ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi, hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri. |
| BSB 17 But now you are laden with the judgment due the wicked; judgment and justice have seized you. | SWKCV 17 Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu; hukumu na haki vimekukamata. |
| BSB 18 Be careful that no one lures you with riches; do not let a large bribe lead you astray. | SWKCV 18 Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri; usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa. |
| BSB 19 Can your wealth or all your mighty effort keep you from distress? | SWKCV 19 Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingi vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki? |
| BSB 20 Do not long for the night, when people vanish from their homes. | SWKCV 20 Usiutamani usiku uje, ili uwaburute watu mbali na nyumba zao. |
| BSB 21 Be careful not to turn to iniquity, for this you have preferred to affliction. | SWKCV 21 Jihadhari usigeukie uovu, ambao unaupenda zaidi kuliko mateso. |
| BSB 22 Behold, God is exalted in His power. Who is a teacher like Him? | SWKCV 22 “Mungu ametukuzwa katika nguvu zake. Ni nani aliye mwalimu kama yeye? |
| BSB 23 Who has appointed His way for Him, or told Him, ‘You have done wrong’? | SWKCV 23 Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake, au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’? |
| BSB 24 Remember to magnify His work, which men have praised in song. | SWKCV 24 Kumbuka kuzitukuza kazi zake, ambazo watu wamezisifu katika wimbo. |
| BSB 25 All mankind has seen it; men behold it from afar. | SWKCV 25 Wanadamu wote wameiona; watu wanaikazia macho kwa mbali. |
| BSB 26 Indeed, God is great—beyond our knowledge; the number of His years is unsearchable. | SWKCV 26 Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, kupita ufahamu wetu! Hesabu ya miaka yake haitafutiki. |
| BSB 27 For He draws up drops of water which distill the rain from the mist, | SWKCV 27 “Yeye huvuta juu matone ya maji, ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito; |
| BSB 28 which the clouds pour out and shower abundantly on mankind. | SWKCV 28 mawingu huangusha chini maji yake, nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu. |
| BSB 29 Furthermore, who can understand how the clouds spread out, how the thunder roars from His pavilion? | SWKCV 29 Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu, jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake. |
| BSB 30 See how He scatters His lightning around Him and covers the depths of the sea. | SWKCV 30 Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka, naye huvifunika vilindi vya bahari. |
| BSB 31 For by these He judges the nations and provides food in abundance. | SWKCV 31 Hivi ndivyo atawalavyo mataifa, na kuwapa chakula kwa wingi. |
| BSB 32 He fills His hands with lightning and commands it to strike its mark. | SWKCV 32 Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi, na kuuagiza kulenga shabaha yake. |
| BSB 33 The thunder declares His presence; even the cattle regard the rising storm. | SWKCV 33 Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja; hata mifugo hujulisha kukaribia kwake. |
Questions about Job 36? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.