Leviticus 11
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 The LORD spoke again to Moses and Aaron, telling them, | SWKCV 1 Bwana akawaambia Mose na Aroni, |
| BSB 2 “Say to the Israelites, ‘Of all the beasts of the earth, these ones you may eat: | SWKCV 2 “Waambieni Waisraeli: ‘Kati ya wanyama wote waishio juu ya nchi, hawa ndio mtakaowala: |
| BSB 3 You may eat any animal that has a split hoof completely divided and that chews the cud. | SWKCV 3 Mwaweza kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua. |
| BSB 4 But of those that only chew the cud or only have a divided hoof, you are not to eat the following: The camel, though it chews the cud, does not have a divided hoof; it is unclean for you. | SWKCV 4 “ ‘Kuna wanyama wengine ambao hucheua tu au wenye kwato zilizogawanyika tu, lakini hao kamwe msiwale. Ngamia ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; kwa kawaida ya ibada hiyo ni najisi kwenu. |
| BSB 5 The rock badger, though it chews the cud, does not have a divided hoof; it is unclean for you. | SWKCV 5 Pelele ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu. |
| BSB 6 The rabbit, though it chews the cud, does not have a divided hoof; it is unclean for you. | SWKCV 6 Sungura ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu. |
| BSB 7 And the pig, though it has a split hoof completely divided, does not chew the cud; it is unclean for you. | SWKCV 7 Naye nguruwe ingawa anazo kwato zilizogawanyika sehemu mbili, hacheui; huyo ni najisi kwenu. |
| BSB 8 You must not eat their meat or touch their carcasses; they are unclean for you. | SWKCV 8 Kamwe msile nyama yao wala kugusa mizoga yao; wao ni najisi kwenu. |
| BSB 9 Of all the creatures that live in the water, whether in the seas or in the streams, you may eat anything with fins and scales. | SWKCV 9 “ ‘Kuhusu viumbe wote wanaoishi ndani ya maji ya bahari na vijito, mtakula wale wote wenye mapezi na magamba. |
| BSB 10 But the following among all the teeming life and creatures in the water are detestable to you: everything in the seas or streams that does not have fins and scales. | SWKCV 10 Lakini viumbe wote ndani ya bahari au vijito wasio na mapezi na magamba, wakiwa miongoni mwa makundi au viumbe wote ndani ya maji, hao ni machukizo kwenu. |
| BSB 11 They shall be an abomination to you; you must not eat their meat, and you must detest their carcasses. | SWKCV 11 Nao watakuwa machukizo kwenu. Msile nyama yao, nayo mizoga yao itakuwa machukizo. |
| BSB 12 Everything in the water that does not have fins and scales shall be detestable to you. | SWKCV 12 Chochote kinachoishi ndani ya maji ambacho hakina mapezi na magamba kitakuwa chukizo kwenu. |
| BSB 13 Additionally, you are to detest the following birds, and they must not be eaten because they are detestable: the eagle, the bearded vulture, the black vulture, | SWKCV 13 “ ‘Wafuatao ndio ndege watakaokuwa machukizo kwenu, hivyo msiwale kwa sababu ni chukizo: tai, furukombe, kipungu, |
| BSB 14 the kite, any kind of falcon, | SWKCV 14 mwewe mwekundu, aina zote za mwewe mweusi, |
| BSB 15 any kind of raven, | SWKCV 15 aina zote za kunguru, |
| BSB 16 the ostrich, the screech owl, the gull, any kind of hawk, | SWKCV 16 mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga, shakwe, aina zote za kipanga, |
| BSB 17 the little owl, the cormorant, the great owl, | SWKCV 17 bundi, mnandi, bundi mkubwa, |
| BSB 18 the white owl, the desert owl, the osprey, | SWKCV 18 mumbi, mwari, nderi, |
| BSB 19 the stork, any kind of heron, the hoopoe, and the bat. | SWKCV 19 korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo. |
| BSB 20 All flying insects that walk on all fours are detestable to you. | SWKCV 20 “ ‘Wadudu wote warukao ambao hutembea kwa miguu minne watakuwa chukizo kwenu. |
| BSB 21 However, you may eat the following kinds of flying insects that walk on all fours: those having jointed legs above their feet for hopping on the ground. | SWKCV 21 Lakini wako viumbe wenye mabawa ambao hutembea kwa miguu minne mtakaowala: wale wenye vifundo katika miguu yao ya kurukaruka juu ya ardhi. |
| BSB 22 Of these you may eat any kind of locust, katydid, cricket, or grasshopper. | SWKCV 22 Miongoni mwa hawa, mtakula nzige wa aina zote, senene, parare au panzi. |
| BSB 23 All other flying insects that have four legs are detestable to you. | SWKCV 23 Lakini viumbe wengine wote wenye mabawa na wenye miguu minne ni machukizo kwenu. |
| BSB 24 These creatures will make you unclean. Whoever touches their carcasses will be unclean until evening, | SWKCV 24 “ ‘Mtajinajisi kwa wanyama hawa. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni. |
| BSB 25 and whoever picks up one of their carcasses must wash his clothes, and he will be unclean until evening. | SWKCV 25 Yeyote atakayebeba mizoga ya viumbe hawa ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. |
| BSB 26 Every animal with hooves not completely divided or that does not chew the cud is unclean for you. Whoever touches any of them will be unclean. | SWKCV 26 “ ‘Kila mnyama mwenye ukwato ulioachana lakini haukugawanyika kabisa, au yule asiyecheua, huyo ni najisi kwenu; yeyote agusaye mzoga wowote wa hao atakuwa najisi. |
| BSB 27 All the four-footed animals that walk on their paws are unclean for you; whoever touches their carcasses will be unclean until evening, | SWKCV 27 Miongoni mwa wanyama wote watembeao kwa miguu minne, wale watembeao kwa vitanga vyao ni najisi kwenu; yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni. |
| BSB 28 and anyone who picks up a carcass must wash his clothes, and he will be unclean until evening. They are unclean for you. | SWKCV 28 Yeyote atakayebeba mizoga yao ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Wanyama hawa ni najisi kwenu. |
| BSB 29 The following creatures that move along the ground are unclean for you: the mole, the mouse, any kind of great lizard, | SWKCV 29 “ ‘Kuhusu wanyama watambaao juu ya ardhi, hawa ni najisi kwenu: kicheche, panya, aina yoyote ya mijusi mikubwa, |
| BSB 30 the gecko, the monitor lizard, the common lizard, the skink, and the chameleon. | SWKCV 30 guruguru, kenge, mijusi ya ukutani, goromoe na kinyonga. |
| BSB 31 These animals are unclean for you among all the crawling creatures. Whoever touches them when they are dead shall be unclean until evening. | SWKCV 31 Hao wote watambaao juu ya ardhi ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mizoga yao atakuwa najisi mpaka jioni. |
| BSB 32 When one of them dies and falls on something, that article becomes unclean; any article of wood, clothing, leather, sackcloth, or any implement used for work must be rinsed with water and will remain unclean until evening; then it will be clean. | SWKCV 32 Ikiwa mmoja wao atakufa na kuangukia juu ya kitu fulani, chombo hicho, hata kikiwa cha matumizi gani, kitakuwa najisi, kiwe kimetengenezwa kwa mti, nguo, ngozi au gunia. Kiweke ndani ya maji; kitakuwa najisi mpaka jioni, kisha kitakuwa safi tena. |
| BSB 33 If any of them falls into a clay pot, everything in it will be unclean; you must break the pot. | SWKCV 33 Ikiwa mmoja wa wanyama aliyekufa ataangukia ndani ya chungu, kila kilichomo katika chungu hicho kitakuwa najisi, nawe ni lazima uvunje chungu hicho. |
| BSB 34 Any food coming into contact with water from that pot will be unclean, and any drink in such a container will be unclean. | SWKCV 34 Chakula chochote ambacho chaweza kuliwa lakini kikawa kimeingia maji kutoka kwenye chungu hicho ni najisi, na kitu chochote cha majimaji ambacho chaweza kunyweka kutoka kwenye chungu hicho ni najisi. |
| BSB 35 Anything upon which one of their carcasses falls will be unclean. If it is an oven or cooking pot, it must be smashed; it is unclean and will remain unclean for you. | SWKCV 35 Chochote ambacho mzoga wa mmojawapo utaangukia kitakuwa najisi. Jiko au chungu cha kupikia ni lazima kivunjwe. Ni najisi, nawe ni lazima uvihesabu kuwa najisi. |
| BSB 36 Nevertheless, a spring or cistern containing water will remain clean, but one who touches a carcass in it will be unclean. | SWKCV 36 Lakini chemchemi au kisima, mahali pa kuchota maji, patakuwa safi, lakini yeyote atakayegusa moja ya mizoga hii ni najisi. |
| BSB 37 If a carcass falls on any seed for sowing, the seed is clean; | SWKCV 37 Kama mzoga ukianguka juu ya mbegu zozote ambazo ni za kupanda, zinabaki safi. |
| BSB 38 but if water has been put on the seed and a carcass falls on it, it is unclean for you. | SWKCV 38 Lakini kama mbegu imetiwa maji na mzoga ukaanguka juu yake, hiyo mbegu ni najisi kwenu. |
| BSB 39 If an animal that you may eat dies, anyone who touches the carcass will be unclean until evening. | SWKCV 39 “ ‘Kama mnyama ambaye mnaruhusiwa kumla akifa, yeyote atakayeugusa mzoga wake atakuwa najisi mpaka jioni. |
| BSB 40 Whoever eats from the carcass must wash his clothes and will be unclean until evening, and anyone who picks up the carcass must wash his clothes and will be unclean until evening. | SWKCV 40 Yeyote atakayekula sehemu ya mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. Yeyote atakayebeba mzoga huo ni lazima afue nguo zake, naye atakuwa najisi mpaka jioni. |
| BSB 41 Every creature that moves along the ground is detestable; it must not be eaten. | SWKCV 41 “ ‘Kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi ni chukizo; kisiliwe. |
| BSB 42 Do not eat any creature that moves along the ground, whether it crawls on its belly or walks on four or more feet; for such creatures are detestable. | SWKCV 42 Msile kiumbe chochote kitambaacho juu ya ardhi, kiwe kitambaacho kwa tumbo lake, au kitambaacho kwa miguu minne au kwa miguu mingi; ni chukizo. |
| BSB 43 Do not defile yourselves by any crawling creature; do not become unclean or defiled by them. | SWKCV 43 Msijitie unajisi kwa chochote katika viumbe hivi. Msijitie unajisi kwa viumbe hivyo au kutiwa unajisi navyo. |
| BSB 44 For I am the LORD your God; consecrate yourselves, therefore, and be holy, because I am holy. You must not defile yourselves by any creature that crawls along the ground. | SWKCV 44 Mimi ndimi Bwana Mungu wenu; jitakaseni mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu. Msijitie unajisi wenyewe kwa kiumbe chochote kile kiendacho juu ya ardhi. |
| BSB 45 For I am the LORD, who brought you up out of the land of Egypt so that I would be your God; therefore be holy, because I am holy. | SWKCV 45 Mimi ndimi Bwana niliyewapandisha mtoke Misri ili niwe Mungu wenu. Kwa hiyo kuweni watakatifu kwa sababu Mimi ni mtakatifu. |
| BSB 46 This is the law regarding animals, birds, all living creatures that move in the water, and all creatures that crawl along the ground. | SWKCV 46 “ ‘Haya ndiyo masharti kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe hai kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kiendacho juu ya ardhi. |
| BSB 47 You must distinguish between the unclean and the clean, between animals that may be eaten and those that may not.’” | SWKCV 47 Ni lazima mpambanue kati ya kilicho najisi na kilicho safi, kati ya viumbe hai vinavyoweza kuliwa na vile visivyoweza kuliwa.’” |
Questions about Leviticus 11? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.