Psalms 30
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 A Psalm. A song for the dedication of the temple. Of David. I will exalt You, O LORD, for You have lifted me up and have not allowed my foes to rejoice over me. | SWKCV 1 Nitakutukuza wewe, Ee Bwana, kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi, na hukuacha adui zangu washangilie juu yangu. |
| BSB 2 O LORD my God, I cried to You for help, and You healed me. | SWKCV 2 Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya. |
| BSB 3 O LORD, You pulled me up from Sheol; You spared me from descending into the Pit. | SWKCV 3 Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. |
| BSB 4 Sing to the LORD, O you His saints, and praise His holy name. | SWKCV 4 Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake; lisifuni jina lake takatifu. |
| BSB 5 For His anger is fleeting, but His favor lasts a lifetime. Weeping may stay the night, but joy comes in the morning. | SWKCV 5 Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha. |
| BSB 6 In prosperity I said, “I will never be shaken.” | SWKCV 6 Nilipofanikiwa nilisema, “Sitatikiswa kamwe.” |
| BSB 7 O LORD, You favored me; You made my mountain stand strong. When You hid Your face, I was dismayed. | SWKCV 7 Ee Bwana, uliponijalia, uliuimarisha mlima wangu, lakini ulipouficha uso wako nilifadhaika. |
| BSB 8 To You, O LORD, I called, and I begged my Lord for mercy: | SWKCV 8 Kwako wewe, Ee Bwana, niliita, kwa Bwana niliomba rehema: |
| BSB 9 “What gain is there in my bloodshed, in my descent to the Pit? Will the dust praise You? Will it proclaim Your faithfulness? | SWKCV 9 “Kuna faida gani katika kuangamia kwangu? Katika kushuka kwangu shimoni? Je, mavumbi yatakusifu? Je, yatatangaza uaminifu wako? |
| BSB 10 Hear me, O LORD, and have mercy; O LORD, be my helper.” | SWKCV 10 Ee Bwana, unisikie na kunihurumia, Ee Bwana, uwe msaada wangu.” |
| BSB 11 You turned my mourning into dancing; You peeled off my sackcloth and clothed me with joy, | SWKCV 11 Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe, |
| BSB 12 that my heart may sing Your praises and not be silent. O LORD my God, I will give thanks forever. | SWKCV 12 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele. |
Questions about Psalms 30? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.