Mark 1
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 This is the beginning of the gospel of Jesus Christ, the Son of God. | SWKCV 1 Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. |
| BSB 2 As it is written in Isaiah the prophet: “Behold, I will send My messenger ahead of You, who will prepare Your way.” | SWKCV 2 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako, atakayetengeneza njia mbele yako”: |
| BSB 3 “A voice of one calling in the wilderness, ‘Prepare the way for the Lord, make straight paths for Him.’” | SWKCV 3 “sauti ya mtu aliaye nyikani. ‘Itengenezeni njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake.’” |
| BSB 4 John the Baptist appeared in the wilderness, preaching a baptism of repentance for the forgiveness of sins. | SWKCV 4 Yohana alikuja, akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi. |
| BSB 5 People went out to him from all of Jerusalem and the countryside of Judea. Confessing their sins, they were baptized by him in the Jordan River. | SWKCV 5 Watu kutoka Uyahudi wote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani. |
| BSB 6 John was clothed in camel’s hair, with a leather belt around his waist. His food was locusts and wild honey. | SWKCV 6 Yohana alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. |
| BSB 7 And he proclaimed: “After me will come One more powerful than I, the straps of whose sandals I am not worthy to stoop down and untie. | SWKCV 7 Naye alihubiri akisema, “Baada yangu atakuja yeye aliye na uwezo kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake. |
| BSB 8 I baptize you with water, but He will baptize you with the Holy Spirit.” | SWKCV 8 Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.” |
| BSB 9 In those days Jesus came from Nazareth in Galilee and was baptized by John in the Jordan. | SWKCV 9 Wakati huo Yesu akaja kutoka Nazareti ya Galilaya, naye akabatizwa na Yohana katika Mto Yordani. |
| BSB 10 As soon as Jesus came up out of the water, He saw the heavens breaking open and the Spirit descending on Him like a dove. | SWKCV 10 Yesu alipokuwa akitoka ndani ya maji, aliona mbingu zikifunguka na Roho akishuka juu yake kama hua. |
| BSB 11 And a voice came from heaven: “You are My beloved Son; in You I am well pleased.” | SWKCV 11 Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.” |
| BSB 12 At once the Spirit drove Jesus into the wilderness, | SWKCV 12 Wakati huo huo, Roho akamwongoza Yesu kwenda nyikani, |
| BSB 13 and He was there for forty days, being tempted by Satan. He was with the wild animals, and the angels ministered to Him. | SWKCV 13 naye akawa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikaa na wanyama wa mwituni, nao malaika wakamhudumia. |
| BSB 14 After the arrest of John, Jesus went into Galilee and proclaimed the gospel of God. | SWKCV 14 Baada ya Yohana kukamatwa na kutiwa gerezani, Yesu aliingia Galilaya akaanza kuhubiri habari njema ya Mungu, |
| BSB 15 “The time is fulfilled,” He said, “and the kingdom of God is near. Repent and believe in the gospel!” | SWKCV 15 akisema, “Wakati umewadia, Ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Habari Njema.” |
| BSB 16 As Jesus was walking beside the Sea of Galilee, He saw Simon and his brother Andrew. They were casting a net into the sea, for they were fishermen. | SWKCV 16 Yesu alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. |
| BSB 17 “Come, follow Me,” Jesus said, “and I will make you fishers of men.” | SWKCV 17 Yesu akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” |
| BSB 18 And at once they left their nets and followed Him. | SWKCV 18 Mara wakaacha nyavu zao, wakamfuata. |
| BSB 19 Going on a little farther, He saw James son of Zebedee and his brother John. They were in a boat, mending their nets. | SWKCV 19 Alipokwenda mbele kidogo, akamwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa kwenye mashua yao wakizitengeneza nyavu zao. |
| BSB 20 Immediately Jesus called them, and they left their father Zebedee in the boat with the hired men and followed Him. | SWKCV 20 Papo hapo akawaita, nao wakamwacha Zebedayo baba yao kwenye mashua pamoja na watumishi wa kuajiriwa, nao wakamfuata Yesu. |
| BSB 21 Then Jesus and His companions went to Capernaum, and right away Jesus entered the synagogue on the Sabbath and began to teach. | SWKCV 21 Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya Sabato, mara Yesu akaingia sinagogi, akaanza kufundisha. |
| BSB 22 The people were astonished at His teaching, because He taught as one who had authority, and not as the scribes. | SWKCV 22 Watu wakashangaa sana kwa mafundisho yake, kwa maana aliwafundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wa sheria. |
| BSB 23 Suddenly a man with an unclean spirit cried out in the synagogue: | SWKCV 23 Wakati huo huo katika sinagogi lao palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, |
| BSB 24 “What do You want with us, Jesus of Nazareth? Have You come to destroy us? I know who You are—the Holy One of God!” | SWKCV 24 naye akapiga kelele akisema, “Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!” |
| BSB 25 But Jesus rebuked the spirit. “Be silent!” He said. “Come out of him!” | SWKCV 25 Lakini Yesu akamkemea, akamwambia, “Nyamaza kimya! Nawe umtoke!” |
| BSB 26 At this, the unclean spirit threw the man into convulsions and came out with a loud shriek. | SWKCV 26 Yule pepo mchafu akamtikisatikisa huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa. |
| BSB 27 All the people were amazed and began to ask one another, “What is this? A new teaching with authority! He commands even the unclean spirits, and they obey Him!” | SWKCV 27 Watu wote wakashangaa, hata wakaulizana wao kwa wao, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya, tena yenye mamlaka! Anaamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!” |
| BSB 28 And the news about Jesus spread quickly through the whole region of Galilee. | SWKCV 28 Sifa zake zikaanza kuenea haraka katika eneo lote la karibu na Galilaya. |
| BSB 29 As soon as Jesus and His companions had left the synagogue, they went with James and John to the home of Simon and Andrew. | SWKCV 29 Mara walipotoka katika sinagogi, walikwenda pamoja na Yakobo na Yohana hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea. |
| BSB 30 Simon’s mother-in-law was sick in bed with a fever, and they promptly told Jesus about her. | SWKCV 30 Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Yesu habari zake. |
| BSB 31 So He went to her, took her by the hand, and helped her up. The fever left her, and she began to serve them. | SWKCV 31 Hivyo Yesu akamwendea, akamshika mkono na kumwinua. Kisha homa ikamwacha, naye akaanza kuwahudumia. |
| BSB 32 That evening, after sunset, people brought to Jesus all the sick and demon-possessed, | SWKCV 32 Jioni ile baada ya jua kutua, watu wakamletea Yesu wagonjwa wote na waliopagawa na pepo wachafu. |
| BSB 33 and the whole town gathered at the door. | SWKCV 33 Mji wote ukakusanyika mbele ya nyumba hiyo. |
| BSB 34 And He healed many who were ill with various diseases and drove out many demons. But He would not allow the demons to speak, because they knew who He was. | SWKCV 34 Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Akawatoa pepo wachafu wengi, lakini hakuwaacha hao pepo wachafu waseme, kwa sababu walimjua yeye ni nani. |
| BSB 35 Early in the morning, while it was still dark, Jesus got up and went out to a solitary place to pray. | SWKCV 35 Alfajiri na mapema sana kulipokuwa bado kuna giza, Yesu akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha ili kuomba. |
| BSB 36 Simon and his companions went to look for Him, | SWKCV 36 Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta, |
| BSB 37 and when they found Him, they said, “Everyone is looking for You!” | SWKCV 37 nao walipomwona, wakamwambia, “Kila mtu anakutafuta!” |
| BSB 38 But Jesus answered, “Let us go on to the neighboring towns so I can preach there as well, for that is why I have come.” | SWKCV 38 Yesu akawajibu, “Twendeni mahali pengine kwenye vijiji jirani, ili niweze kuhubiri huko pia, kwa sababu hicho ndicho nilichokuja kukifanya.” |
| BSB 39 So He went throughout Galilee, preaching in their synagogues and driving out demons. | SWKCV 39 Kwa hiyo akazunguka Galilaya kote, akihubiri katika masinagogi yao na kutoa pepo wachafu. |
| BSB 40 Then a leper came to Jesus, begging on his knees: “If You are willing, You can make me clean.” | SWKCV 40 Mtu mmoja mwenye ukoma alimjia Yesu, akamwomba akipiga magoti, akamwambia, “Ukitaka, waweza kunitakasa.” |
| BSB 41 Moved with compassion, Jesus reached out His hand and touched the man. “I am willing,” He said. “Be clean!” | SWKCV 41 Yesu, akiwa amejawa na huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka. Takasika!” |
| BSB 42 And immediately the leprosy left him, and the man was cleansed. | SWKCV 42 Mara ukoma ukamtoka, naye akatakasika. |
| BSB 43 Jesus promptly sent him away with a stern warning: | SWKCV 43 Baada ya Yesu kumwonya vikali, akamruhusu aende zake |
| BSB 44 “See that you don’t tell anyone. But go, show yourself to the priest and present the offering Moses prescribed for your cleansing, as a testimony to them.” | SWKCV 44 akimwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote habari hizi, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka alizoagiza Mose kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.” |
| BSB 45 But the man went out and openly began to proclaim and spread the news. Consequently, Jesus could no longer enter a town in plain view, but He stayed out in solitary places. Yet people came to Him from every quarter. | SWKCV 45 Lakini yule mtu akaenda akaanza kutangaza habari za kuponywa kwake waziwazi. Kwa hiyo, Yesu hakuweza tena kuingia katika miji waziwazi lakini alikaa sehemu zisizo na watu. Hata hivyo watu wakamfuata huko kutoka kila upande. |
Questions about Mark 1? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.